Msaada mtoto anakakamaa shingo

Loeli

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2014
Posts
997
Reaction score
763
Wakuu nilileta post hapa jana ya mtoto mzazi alikosea akaoverdose amoxylin capsule. Ana miaka 8. Walimchemshia maziwa na alipokunywa ghafla shingo ikaanza kukakamaa na ikawa inafanya hivyo kila say nusu saa. Wakamkimbiza Hindu Mandal. Daktari akawaambia hakukuwa na tatizo la overdose. Na kuwa kukakamaa shingo haitokani na dawa hizo. Waneshindwa kuona ugonjwa na wamemoa referal aende amana hosp ili apate referal ya muhimbili. Wataalam tusaidieni please. Tuko katika panic maana hata homa hana na akishaanza kukakamaa jasho mwili mzima
 
Je hivi sasa mpo Amana, Muhimbili, Hindu Mandal au nyumbani? Ni muhimu mkampeleka mtoto huko mlipopewa referral kwa ajili ya uchunguzi zaidi!

Mimi pia sidhani kama kukakamaa kwa shingo kuna sababishwa na amoxycillin overdose. Hiyo ni shida nyingine ambayo imekuja coincidentally baada ya amoxycillin overdose na inahitaji uchunguzi wa kina!
 
Mkuu, ngoja wataalam waje ila la kuomba mungu no afike hospital mapema iwezekanavyo
 

Asante sana mkuu. Tunafuatilia nitaleta mrejesho.
 

Wazazi walimrudisha nyumbani kwa maombi maana inaonekana Hindumandal kuna mhindi mmoja mzee aliwashauri watafute mtu wa maombi sambamba na hospital. Sijawasiliana nao tena nijue walikofikia. Nitafuatilia.
 
Ana miaka miangapi, wa lkike au wa kiume. For me possible ni degedege au sydehams chorea secondary to rheumatic fever. Sasa Hindu Mandal wanashindwa hata kutoa initial dx kutoa panic kwa mzazi. Au Hindu Mandal wa clinical Officers na AMO. Pole sana nenda huko amana yupo Dr Andrew pale ingawa weekends imnaweza isiwe rahisi kumpata
 

Anatimiza miaka 8 1st May. Hakika nilikuwa na wazazi na waluokuwepo you could tell ni junior sana, possible hata interns bado. Hawakutoa dawa zaidi ya massage ya shingo na kusema hawaoni tatizo. Nilishangaa.
 
Nahisi hiyo ni degedege sina hakika kama hospital wanaweza kukusaidia haraka ila tiba mbadala ni swala la siku moja
 

Mkuu dr Barca degedege inashika na 8 years? sifahamu kabisa masuala haya. Hana homa kabisa. Ila tarehe 24 ndiyo aliugua na homa kali na kutapika akapelekwa temeke na kupata amoxycillin. Hakua na malaria. Hata jana Hindu mandal hakukutwa na malari na full blood picture ilikuwa ok except some protin trace. Ilikuwa mchana. Na saa 8 alipewa dose yake ya amoxycillin ila sasa mzazi alipokuwa anampa dawa saa 12 jioni ya anti vommitting akasahau akampa tena amoxyllin. Mama aliporudi after an hour mume akaeleza kilichotokea na immediately akachemsha maziwa ya ng'ombe akampa akanywa na kabla hajamaluza ndiyo shingo ikaanza kwenda upande. Ilianzia kulia kwenda kushoto. Baadaye ikawa inatizama juu tu kwa nguvu na ikianza jasho kubwa na nguvu kubwa sana alikuwa anatumia.
 
Mkuu japo mimi si daktari lakini tatizo la mtoto wako lipo kwenye ubongo .kuna daktari mmoja sina uhakika sana na jina lake lakini anapatikana karibu regency hospital ana clinin yake nadhani ukienda pale utapata solution
 
Nahisi hiyo ni degedege sina hakika kama hospital wanaweza kukusaidia haraka ila tiba mbadala ni swala la siku moja

Mkuu mtunzasiri funguka tusaidie hiyo tiba mbadala inapatikana waoi tukimbilie huko. Please help tunaomba.
 
Mkuu japo mimi si daktari lakini tatizo la mtoto wako lipo kwenye ubongo .kuna daktari mmoja sina uhakika sana na jina lake lakini anapatikana karibu regency hospital ana clinin yake nadhani ukienda pale utapata solution

Asante mkuu. Sijakuelewa vizuri. Unasema yuko regency hosp na ana private clinic au private clinic ndiyo iko jirani na regency? please please
 
Asante mkuu. Sijakuelewa vizuri. Unasema yuko regency hosp na ana private clinic au private clinic ndiyo iko jirani na regency? please please
Ana clinic yake binafsi ipo karibu na regency kwa kweli sina uhakika na jina ni prof wa muhimbili ,ukiwa regency kama unaelekea Njia ya kwenda jangwani mita chache kutoka hapo regency mkono wa kulia kuna njia inachepuka na kuna daycare kubwa nina uhakika ukiulizia utapata mtu wa kukuonesha
 

Asante sana mkuu. Ubarikiwe sana. Tunajiyahidi kila upande na maombi kwa Mungu. Kwa sasa tangu saa tisa usiku tatizo halijatokea tena sema uchovu na kutapika japo si sana. Kwa imani ya wazazi maombi yalisaidia sana. Muhimbili kwa leo weekend sijajua mafanikio. Naona tutaenda hapo kwa prof regency ili kama ct scan tufanye leo. Maana hata Muhimbili wakituandikia ct scan kwanza sina hakika kama inafanya kazi na pili si zile appoitntment zao. Ct scan ya kisasa tutaipata wapi mkuu?.kati ya aghakan na regency?
 
Mkuu MziziMkavu njoo saidia tiba mbadala ya shingo kukakamaa. Ushauri wamesema kwa kuanzia tupige degedege huku tukienda vipimo vya ct scan.
 
hapo kipimo cha kujua ugonjwa ni wa tiba mbadala au ni hospital ikitokea hilo degedege chukua kitunguu saum kiponde mnusishe puani ikiacha haraka hilo degedege ujue tiba mbadala likiendelea haraka hospital
 

zipo aina nyingi sana za degedege si lazima itokee ile unayoifahamu ya kukakamaa mwili mzima, zipo nyingine zinaweza husisha just kiungo kimoja cha mwili, mimi kwa mtazamo wangu ingawa nipo mbali yawezekana ana shida mojawapo kati ya hizi kwanza conlvusions au degedege na hii inaweza tokea kwa umri wowote kikubwa ni kutafuta nini chanzo cha hiyo degedege. pili hii inawezekana ni homa ya mifupa ambayo ni very common to this age na hii sign tunaita sydehams chorea. vipimo ambavyo mimi ningefanya kwa harakaharaka ni ASOT yaan antistreptolysin O titre, EEG, lakini pia sukari. mbali na hayo ningetoa angalau hata dawa ya kupunguza kukakamaa huko. Dr kusema haoni tatizo wakati mtoto anaonekana anatatitzo is not fare honest. coz hiyo ni abnormal presentation. Sasa napenda kujua so far ameshapata huduma gani hadi sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…