Msaada: Mtoto ananyonya sana

Msaada: Mtoto ananyonya sana

Habar

Ndugu zangu nina mtoto wa kiume wa miezi 3 ananyonya sana mpaka mama yake anachoka na hashibi, ukimtoa analia.

Na clinic wameshaur mtoto anyonye tu maziwa ya mama hadi afikishe miezi 6

Nini naweza kufanya kumsaidia mtoto na mamake?
Hakikisha mama anakula chakula Cha kutosha so chini ya milo 5 Kwa siku
 
Kiongozi
Inaelekea mama hana maziwa ya kutosha. Jitahidi mama ale vitu vya kumuongezea maziwa.
Kama bajeti haiko vizuri kununua hayo maziwa ya formula, Mwanzishie maziwa ya ngombe (una weka nusu maziwa na nusu maji) mf: unachanganya kikombe kimoja maziwa na kikombe kimoja maji ili yawe mepesi kabisa. Na ikiwezekana upate mtu mwenye ngombe kabisa ili akupe maziwa ya ngombe mmoja (asibadilishe badilishe ngombe) wafugaji wanajua ukimwambia maziwa ya mtoto
Akinywa hayo maziwa yaliyo changanywa na maji akiteremshia na ya mama atakuwa poa kabisa.....
Maziwa ya ng'ombe hapana mkuu. Bado mdogo sana. Atafute ua kopo na ahakikishe siyo feki. Na pia ya kopo anatakiwa ajuwe kuna ya umri tofauti tofauti. All in all, watoto wa kiume wananyonya sana hivyo mama ale vizuri sana kama wengi walivyoshauri.
 
Habar

Ndugu zangu nina mtoto wa kiume wa miezi 3 ananyonya sana mpaka mama yake anachoka na hashibi, ukimtoa analia.

Na clinic wameshaur mtoto anyonye tu maziwa ya mama hadi afikishe miezi 6

Nini naweza kufanya kumsaidia mtoto na mamake?
Mkuu unamuonea wivu mtoto kunyonya matiti ya mke wako? Kwanini usimbumilie tu?
 
Back
Top Bottom