Hayo maelezo yako ndio yanayopelekea tudhani kuna kesi hapo...hakuna mtu utakayempa maelezo hayo alafu akwambie 'wewe huna makosa nenda'
Kujigonga mpaka kupoteza maisha basi huenda kulikuwa na nguvu kubwa iliyosababisha mtoto kupata madhara makubwa..sasa je alisukumwa na mwenzake? alijigonga mwenyewe? madhara aliyapata baada tu ya kujigonga au alijigonga na kuangukia kitu chini? alifariki baada ya muda gani toka aumie?
Nadhani kuna mengi jamuhuri ingependa kufahamu kuona kama gari na mmiliki wake wana mchango, kabla ya kuona uhusiki..hao Wazazi hawahusiki tena hapa, ingawa watahitajika kutoa ushahidi huko mahakamani.