Msaada: Mtoto kazaliwa kichwa kimebonyea upande mmoja

americana

Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
84
Reaction score
37
Ni wiki sasa tangu nijaliwe mtoto wa kwanza, toka alipozaliwa daktari akaniambia mama alimminya mtoto wakati akimpush hadi kupelekea kichwa kubonyea upande mmoja wa kushoto juu ya sikio upande wa kulia. Nimejaribu kuuliza watu wanadai ni hali ya kawaida itakaa sawa tu japo wengine wanashauri niombe msaada wa madaktari kujua tatizo. Kwa kuwa JamiiForum ni sehemu yenye watu wengu wa aina tofauti naombeni mwenye uelewa zaidi au alishaona kitu kama hiki anielekeze vizuri. Tunamkanda kila siku lakini nahisi bado tu.

Asanteni
 

Mpeleke hospitali ya CCRBT iko mkoa wa dar es salaam eneo la Msasani kama sikosei watakusaidia
 
Kama daktari bingwa amesema hakuna shida sioni shida, na sielewi kwa nini mnamkanda kwani nani kawaambia akikandwa kitakuwa sawa, na je hiyo ni scientific; msije mkaongeza tatizo au kuleta tatizo.

Mkimlaza mara nyingi kwa namna fulani kinaweza kuwa sawa, ila nafikiri alipozaliwa tu ilibidi kukisawazisha kwani skull huwa inakuwa bado soft.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…