Ni wiki sasa tangu nijaliwe mtoto wa kwanza, toka alipozaliwa daktari akaniambia mama alimminya mtoto wakati akimpush hadi kupelekea kichwa kubonyea upande mmoja wa kushoto juu ya sikio upande wa kulia. Nimejaribu kuuliza watu wanadai ni hali ya kawaida itakaa sawa tu japo wengine wanashauri niombe msaada wa madaktari kujua tatizo. Kwa kuwa JamiiForum ni sehemu yenye watu wengu wa aina tofauti naombeni mwenye uelewa zaidi au alishaona kitu kama hiki anielekeze vizuri. Tunamkanda kila siku lakini nahisi bado tu.
Asanteni
Asanteni