Wadau habari zenu,nakuja tena hapa jukwaani kuomba msaada wenu kwa masahibu yanikutayo!nina mwanangu ana umri wa miaka miwili sasa,cha ajabu kila ifikapo usiku,hasa kuanzia saa tatu,uwa analia sana tena sana kwa kilio cha ajabu kwa muda hata wa masaa mawili mpaka matatu hivi,uwa pia analia kama vile kuna kitu kinamtisha na anajaribu kupambana nacho!tumempeleka hospital lakini hakuna kitu chochote kilichogunduliwa,hapa kichwa kinaniuma wandugu,sijui hata nianzie wapi na niishie wapi,naombeni ushauri wenu ndugu zangu!
Mkuu.Kapuku83 kuna vitu vibaya ndani ya nyumba yenu vinamtisha ndio anapiga makele mtoto wenu fanya hivi jaribu kununuwa dawa moja inatwa Mvuje na upate na kitunguusaumu punje moja na kipande cha mkaa kimoja vitu vyote hivyo viwe vidogo vidogo funga katika kitambaa cheusi mfunge mkononi huyo mtoto. Na pia usimlaze giza mtoto wewe unapenda kumlaza giza ana inamiwa na pepo mbaya usiku huyo mtoto wako na chini ya mto wake huyo mtoto muwekee kisu kisichokuwa na mpini na ndimu moja na mkaa kipande kimoja fanya hivyo na uwe unamuombee dua kila usiku kisha uje unipe feedback.
Pole kwa ilo jambo ndugu yetu,najua kama mzazi utakua unaumia sana juu ya ilo,ushauri wangu ni kua,hii dunia ina mambo mengi sana mkuu,tembea ujionee,na hata haya mambo ya giza pia yapo japo hatuya amini sana,jaribu kuhangaika na mtoto upande mwingine pia mbali ya hospital pekee!jaribu kwa mapadri,masheikh na hata "wataalam" pia,kikubwa usimdhuru mtu
Mwanao analilia jina la mzazi mmoja wapo toka upande wa kiumeni. Kama ni Mtoto wa Kiume Mwite kwa jina na Baba yake Mumeo au kama ni mtoto wa kike mwite kwa jina la Mama yake Mumeo huwezi kuamini atanyamaza moja kwa moja na hayo ndiyo majina ambayo mtayatumia mara kwa mara ili asirudie kulia lia.
Mmejaribu kumpeleka kwenye maombi?