Wadau habari zenu,nakuja tena hapa jukwaani kuomba msaada wenu kwa masahibu yanikutayo!nina mwanangu ana umri wa miaka miwili sasa,cha ajabu kila ifikapo usiku,hasa kuanzia saa tatu,uwa analia sana tena sana kwa kilio cha ajabu kwa muda hata wa masaa mawili mpaka matatu hivi,uwa pia analia kama vile kuna kitu kinamtisha na anajaribu kupambana nacho!tumempeleka hospital lakini hakuna kitu chochote kilichogunduliwa,hapa kichwa kinaniuma wandugu,sijui hata nianzie wapi na niishie wapi,naombeni ushauri wenu ndugu zangu!