MSAADA: Mtoto wa miaka minne anachemka sana kwa siku tatu mfululizo. Hospitali alipimwa malaria, hana

Joined
May 8, 2020
Posts
93
Reaction score
327
Habarini wakuu, poleni kwa majukumu.

Huyu mtoto alianza kuchemka(joto kupanda sana) Jumamosi usiku wa Septemba 7. Jumapili tulimpeleka Zahanati akapimwa Malaria, hamna.

Dokta akasema itakuwa ni mafua tu labda ndio inayopandisha joto. Tulipatiwa amoxylin, cetrizen na paracetamol.

Ila joto halijashuka kabisa tangu aanze kutumia dawa. Hapa shida inaweza kuwa nini wakuu?

NB: Mtoto hana maumivu ya kichwa. Hajapoteza hamu ya kula, haisi kichefuchefu na hatapiki. Anacheza vizuri ila shida ni hili joto kupanda sana na halitaki kushuka.
 
Nashauri, afanyiwe kipimo cha FULL BLOOD PICTURE na ESR pia. Huenda tukajuwa pa kuanzia.

Na je, alipo enda hospital alipimwa joto la mwili ? Na lilikuwa ni ngapi ???
 
Nakushukuru sana.Hakupimwa joto la mwili.Ni maneno ya mdomoni tu kuwa apimwe malaria na akapimwa.
 
Habarini wakuu.Poleni kwa majukumu.

Huyu mtoto alianza kuchemka(joto kupanda sana) jumamosi usiku wa septemba 7.Jumapili tulimpeleka zahanati akapimwa malaria,hamna.Dokta akasema itakuwa ni mafua tu labda ndio inayopandisha joto.
Tulipatiwa amoxylin,cetrizen na paracetamol.

Ila joto halijashuka kabisa tangu aanze kutumia dawa.Hapa shida inaweza kuwa nini wakuu?.

NB:Mtoto hana maumivu ya kichwa.

Hajapoteza hamu ya kula,haisi kichefuchefu na hatapiki.Anacheza vizuri ila shida ni hili joto kupanda sana na halitaki kushuka.
Joto kali la mwili kuua haraka, rudisha mtoto hospitali awekewe drip wakati diagnosis nyingine zinafanyika, ukimrudisha nyumbani utakua umemuua mwenyewe
 
Nakushukuru sana.Hakupimwa joto la mwili.Ni maneno ya mdomoni tu kuwa apimwe malaria na akapimwa.
Sawa, mpeleke hospital na sio dispensary.

Hakikisha anapimwa joto la mwili, full blood picture, esr na hata blood sugar .

Kuna baadhi ya wahudumu wa Afya huchukulia mambo ki wepesi sana. Rudi hospital mtoto akatibiwe upya.
 
Basi namrudisha tena hospitali.Tupo nyumbani kwa sasa.Ahsante
Jitahidi sanaa dakitari ampe treatment ya kushusha joto la kuchemka na aendelee kumstudy angalao kwa masaa 12. Wakati uchunguzi wa magonjwa mengine yana endelea, usikubali kutudi nyumbani mpaka pale utakavo ona joto limeshuka kabisa.
 
Ndugu hilo tatizo la joto mda wote kwa mtoto sio la kupuuza na kukaa nyumbani, kuna rafiki yangu mtoto wake alifariki kwa hali kama hiyo, mimi pia ilitokea kwa mtoto wangu, madaktari kila wakipima hawaoni kitu, nashukuru sana madaktari wa Bochi hospital wakashauri mtoto apewe dawa za Malaria kwahyo akaanzishiwa hiyo dose, kumbe alikuwa na Malaria iliyojificha, wakati mwingine Malaria ikipimwa haionekani, nakushauri mpeleke hospital kubwa kubwa mwanao usimpeleke zahanati hizi, kama upo dar mpeleke Bochi nawaamini ila ujipange hela kama hauna bima
 
Mimi kwa kawaida huwa siamini majibu ya hospital moja. Mpeleke hospital nyingne apimwe tena. Pia kuna kidonge huwa kinaingizwa kwenye makalio kinashusha homa fasta. Ukikosa nunua ibumex iko njema sana.
Homa huwa inakausha damu.
 
Hiyo ni nzuri, ni paracetamol suppository. Huwa inasaidia sana
 
Habarini wakuu.Poleni kwa majukumu.

Huyu mtoto alianza kuchemka(joto kupanda sana) jumamosi usiku wa septemba 7.Jumapili tulimpeleka zahanati akapimwa malaria,hamna.Dokta akasema itakuwa ni mafua tu labda ndio inayopandisha joto.
Tulipatiwa amoxylin,cetrizen na paracetamol.

Ila joto halijashuka kabisa tangu aanze kutumia dawa.Hapa shida inaweza kuwa nini wakuu?.

NB:Mtoto hana maumivu ya kichwa.

Hajapoteza hamu ya kula,haisi kichefuchefu na hatapiki.Anacheza vizuri ila shida ni hili joto kupanda sana na halitaki kushuka.
Check blood infections
Check blood count.

Utakuja kunishukuru baadae.
 
Sawa, mpeleke hospital na sio dispensary.

Hakikisha anapimwa joto la mwili, full blood picture, esr na hata blood sugar .

Kuna baadhi ya wahudumu wa Afya huchukulia mambo ki wepesi sana. Rudi hospital mtoto akatibiwe upya.
Ahsante sana.Nampeleka hospitali ya wilaya muda huu
 
Yaani bila shaka ni hiyo blood infection, na Kama kipimo cha damu nilicho shauri hapo juu kitaonesha seli nyeupe za damu ziko juu sana basi huenda ikalazimu awe admitted na kuanzishiwa sindano.

Naomba baada ya kurudi naye hospital utuletee mrejesho hapa.
 
Nitawapa mrejesho.Ahsante
 
Kuna wazazi hamko serious na afya za watoto wenu.
 
Ndugu hilo tatizo la joto mda wote kwa mtoto sio la kupuuza na kukaa nyumbani, kuna rafiki yangu mtoto wake alifariki kwa hali kama hiyo, mimi pia ilitokea kwa mtoto wangu, madaktari kila wakipima hawaoni kitu, nashukuru sana madaktari wa Bochi hospital wakashauri mtoto apewe dawa za Malaria kwahyo akaanzishiwa hiyo dose, kumbe alikuwa na Malaria iliyojificha, wakati mwingine Malaria ikipimwa haionekani, nakushauri mpeleke hospital kubwa kubwa mwanao usimpeleke zahanati hizi, kama upo dar mpeleke Bochi nawaamini ila ujipange hela kama hauna bima
Nipo Mwanza mkuu.Nilimpeleka zahanati.Ila kwa sasa nipo njiani naenda nae sekou_toure
 
Back
Top Bottom