Msaada: Mtoto wa mwaka mmoja kutokwa na vipele vidogodogo vigumu

Chronixx1

Member
Joined
Jul 23, 2017
Posts
57
Reaction score
81
Mtoto wangu ana mwaka mmoja na miezi kadhaa. Anatokewa na vipele vidogo vidogo halafu vigumu. Nimejarbu kumpleka hospitali zaidi ya 3 napewa dawa ya kupaka lakini sioni matumaini.

Kwa wanaojua dawa tafadhal naomba mnisaidie !
 
Ajaribu apake BBE mara moja mwili mzima halafu atumie betamethasone cream mara mbili kwa 7/7
 
Tunaeza kuona picha tafadhali,,maana magonjwa ya ngozi yanafanana
 
Mimi sio daktari ila naelewa lazima kuna reason ya vipele kutoka. Chunguza,
1. Je ni mafuta mnayompaka?
2. Ni sabuni ya kufulia nguo inampa shida au sabauni ya kuogea?
3. Ni maziwa ya ng'ombe?
4. Kuna kitu mnaweka kwenye uji ambacho kinamkataa kama karanga?

Usipojua issue ni nini, kutumia dawa ni kazi ya bure.

Lakini pia nenda hospitali, omba kuonana na dermatologist, huyo ndiye anaweza kukupa msaada. Haishauriwi kumpaka mtoto madawa makali ya ngozi. Jaribu kuligundua tatizo kwanza.
 
Mtoto wangu ana mwaka mmoja na miezi kadhaa. Anatokewa na vipele vidogo vidogo halafu vigumu. Nimejarbu kumpleka hospitali zaidi ya 3 napewa dawa ya kupaka lakini sioni matumaini.

Kwa wanaojua dawa tafadhal naomba mnisaidie !
Pole sana kuna mafuta nilikuwa nayanunua sana Kampala kipindi cha nyuma yanaitwa "Skin guard" hebu yatafute, kama unaishi Dar nenda kituo cha mabasi ya Kampala agiza mtu akuletee hata nusu dazani. Naamini utakuja kutoa mrejesho wenye faraja
 
Kuna kitu kinaweza kuwa kinamkataa,either chakula,au mazingira aliyopo iwe nje ama ndani ya nyumba yanaweza kuleta reaction inayopelekea hali hiyo na ikitokea hivyo ndo unatumia dawa na dawa bila matokeo,
kama hujagundua kuwa ni allerge.

Vipi anajikuna sana?
 
Mtoto wangu ana mwaka mmoja na miezi kadhaa. Anatokewa na vipele vidogo vidogo halafu vigumu. Nimejarbu kumpleka hospitali zaidi ya 3 napewa dawa ya kupaka lakini sioni matumaini.

Kwa wanaojua dawa tafadhal naomba mnisaidie !
Tafuta Elocon cream &ointment, mpake pamoja na Enat skin care, utapata matokeo ndani ya masaa macheche au siku 1.
Karibu
 
nisha mshudia mara moja tu anajikuna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…