Msaada mtoto wangu ana upungufu wa damu

Valmg

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2018
Posts
557
Reaction score
838
Habari za usiku, tafadhali naomba ushauri, mwanangu ana miezi nane alizaliwa na damu 16 ila alipimwa tena akiwa na miezi 4 zilikuwa 14 gafla mwezi wa 7 zikawa damu 8 leo kapimwa tena akiwa na miezi8 damu ipo 7. hana tatizo na aumwi chochote anakula na kunyonya vizuri na uzito wake unapanda vizuri, msaada waungwana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko hospitali baada ya kupima uliambiwa nn? Tuanzie hapo kwanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
vipimo vingine vinasemaje?Hospital walikwambia nin


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Akapate kipimo cha Malaria .... Pia kuna kinywaji kinaitwa RIBENA ni kizuri nimeponeaga hicho aisee .... Nimewekewa Chupa 14 za damu enz hizo na 7-8 years old ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
First Aid kama unanyonyesha kifuani, kula maini na red meat, pika mchicha weka nyanya fresh nyingi kula na pamoja na nyama. Ukimaliza kula tu kula machungwa na mananasi. Mtoto atapata iron kutoka kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…