Salaam wana JF
Nina mtoto wa kike wa miaka 5
Kwa muda mrefu huyu dogo hapendi kula ingawa vyakula kibao vyenye lishe anapewa
Mtoto anaishi na mamake mi Niko nae mbali yani nipo mkoa mwingine.
Leo mamake ananipigia simu analalamika mtoto hataki kula na hii kesi haijaanza Jana wala juzi mtoto hapendi kula
Ana uzito wa kg 15 muda mrefu sasa haongezeki, ni mwembamba but suala la kuugua ni nadra sana kwake
Sasa wataalam mnisaidie nifanyaje au mamake afanyaje ili huyu mtoto apende kula? Mamake analalamika kamshindwa kumlazimisha kula
Msaada tafadhali.