Msaada: Mtoto wangu hapendi kula kabisa

Msaada: Mtoto wangu hapendi kula kabisa

Mzee Mchochezi

Senior Member
Joined
Apr 3, 2018
Posts
125
Reaction score
242
Salaam wana JF

Nina mtoto wa kike wa miaka 5

Kwa muda mrefu huyu dogo hapendi kula ingawa vyakula kibao vyenye lishe anapewa

Mtoto anaishi na mamake mi Niko nae mbali yani nipo mkoa mwingine.

Leo mamake ananipigia simu analalamika mtoto hataki kula na hii kesi haijaanza Jana wala juzi mtoto hapendi kula

Ana uzito wa kg 15 muda mrefu sasa haongezeki, ni mwembamba but suala la kuugua ni nadra sana kwake

Sasa wataalam mnisaidie nifanyaje au mamake afanyaje ili huyu mtoto apende kula? Mamake analalamika kamshindwa kumlazimisha kula

Msaada tafadhali.
 
Pole sana jaribu kwenda hospital kwa matibabu zaidi
 
Jitahidi kumpeleka hospitali aonane na Dr wa watoto, pamoja na wataalam wa lishe watakupa ushauri mzuri nini kifanyike, na pengine watachukua vipimo vyingi tu kuangalia tatizo liko wapi.

Mara nyingi hii ya kutokula huja kupotea huko mbeleni kadri mtoto anavyokuwa, cha muhimu upate uwangalizi wa wataalam kwa karibu zaidi.
 
Pole mkuu watoto wanasumbua sana mimi nina kijana wangu hapendi kula tangu ana mwezi hata kunyonya ilikuwa shida kutapika kwa sana akiona chakula tu ni shida now ana miaka 3 nina km two weeks hivi kuna dr alinipa dawa ya vitamins inaitwa pharmactin sina hakika km nimepatia spellings,but nimempa sasa hivi anakula km mchwa kila kitu hakimpiti usiku nalala na chupa ya maziwa anapata njaa bala jaribu hiyo dawa
 
Salaam wana JF

Nina mtoto wa kike wa miaka 5

Kwa muda mrefu huyu dogo hapendi kula ingawa vyakula kibao vyenye lishe anapewa

Mtoto anaishi na mamake mi Niko nae mbali yani nipo mkoa mwingine.

Leo mamake ananipigia simu analalamika mtoto hataki kula na hii kesi haijaanza Jana wala juzi mtoto hapendi kula

Ana uzito wa kg 15 muda mrefu sasa haongezeki, ni mwembamba but suala la kuugua ni nadra sana kwake

Sasa wataalam mnisaidie nifanyaje au mamake afanyaje ili huyu mtoto apende kula? Mamake analalamika kamshindwa kumlazimisha kula

Msaada tafadhali.
Hii ni dalili ya upungufu wa vitamin B Complex iliyopelekea (SPLEEN) kufanya kazi chini ya kiwango na kuweza kusababisha
1. Kushuka kwa kinga ya mwili (degradation of immunity)
2. Kupungua kwa kiwango cha seli nyekundu za damu na kusababisha Anemia
3. Tumbo kujaa gesi
4. Mwili kushindwa kuvyonza virutubisho vya vyakula na kusababisha utapiamlo
5.kushindwa kumeng'enywa kwa chakula na kufanya kitoke vile vile ( undigested food as waste products

6. Lipsi ya chini katika mdomu kuwa na vidonga au kuwa na rangi ya zambarau

USHAURI

Tafuta vitamin B complex supplement hasa zile zenye mchanganyiko mbalimbali wa vitamin.

Mpe matunda yenye radha ya uchachu kama vile chungwa,malimao, ndimu nk.
 
  • Thanks
Reactions: Cyb
Jamani kweli palipo na wengi hapakosi kitu. Mi mwenyewe nina binti yangu ana miaka miwili na nusu sasa. Hapendi kula, anaweza kushinda siku nzima pasipo kutaka kula. Nimeshajaribu kumpatia matunda tofauti lakini wapi; atakula vipande viwili tu kisha anaenda zake kucheza. Wataalamu tusaidieni pls
 
Back
Top Bottom