msaada muhimu sana:kwa binti huyu aliyefanyiwa abortion ya lazima

msaada muhimu sana:kwa binti huyu aliyefanyiwa abortion ya lazima

iron finger

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
358
Reaction score
220
wakuu naomba busara zenu.

juzi majira ya usiku maeneo ya kigamboni nikiwa natoka kwenye mizunguko yangu maeneo ya kigamboni mbele yangu nikamuona binti mdogo akiugulia maumivu ya tumbo alikuwa na bwana.wake nilienda kutoa msaada haraka na kufika yule mume wa binti akaniambia kuwa mkewe ni mjamzito wa miezi mitano na ameanza kuumwa tumbo mda huo kwa mujibu wa maelekezo ya yule bwana walikuwa wanatokea kwenye mizunguko yao yeye na mkewe ndipo hali ile ya kuumwa tumbo ikaanza
wakati tupo pale yule binti akaanza kutokwa na damu sehemu za siri ikabidi tuchukue tahadhari ya haraka kwa kumuwahisha zahanati ya karibu ili apate huduma ya kwanza(jina la zahanati kapuni)
baada ya kufika pale alipokelewa na nesi mmoja ambaye alikuwa amevaa suruali nyeusi ya kubana na jezi ya chelsea juu na kijana.mmoja mfupi mweupe yeye alivaa suruali ya rangi ya kahawia na tshirt nyeupe yenye michirizi mieusi
walichokifanya ni kumchukua na moja kwa moja kumkimbizia maabara na kutusihi sana sisi tubaki nje baada ya nusu saa nesi alianza kutoka nje na kuchukua vifaa vingi kama kama mikasi,glovs,dripu,za maji na vifaa vyote ambavyo vinaonekana ni vya opereshani
nilishtuka ila sikupenda kumweleza mwenye mke ambaye alishapanic
lakini yule dakatari alitoka nje na kutusihi tutulie
ilipita tena nusu saa bila taarifa yeyote ndipo yule doctar akatoka tena na kutoa taarifa kuwa mgonjwa atajifungua ila mtoto atakufa
nilishtushwa na mwenendo wa yule daktari na kugundua kuwa alikuwa kama amekunywa kidogo
walijitahidi kumfosi yule binti azae kwa kumpa dripu la uchungu na pua chai ya moto ambayo nesi aliniomba mimi niichemshe kwa kutumia heater yao na mama akapewa
baada ya lisaa limoja ilikuja taarifa kuwa mama amejifungua mtoto njiti akiwa hai zilikuwa ni taarifa.zenye mshtuko na mkanganyiko kupokea sasa kesi inakuja kama ifuatavyo

1.kawaida ya mama mjamzito akijifungua daktari anapaswa kuandika ripoti ya kujifungua kwenye kadi ya mama ila huyu alikataa
2.kawaida ya mtoto njiti anapaswa kupelekwa hospita ya taifa ya muhimbili ila daktari alikataa na kutoa ushauri kwa mama aende na mtoto nyumbani akamlee kwa kumvika maguo mazito
3.nesi alisema mgonjwa.aondolewe haraka pale ili afanye usafi bila kujali hali ya mgonjwa
4.kwenye malipo baba aliambiwa atoe 58000/= ya dawa
5.elfu 30 kwa ajili ya mzalishaji nesi na daktari
6.elfu 5 kwa ajili ya kumpa.mlinzi na ili akae kimya asifungue mdomo juu ya kilichotokea
na pia walishindwa kuandika ripoti yeyote juu ya kuwepo kwa mjamzito aliyejifungua

kilichoendelea ni kuwa kile.kichanga kilikaa masaa zaidi ya matatu bila huduma mpaka baade tulipoamua kwenda hospital ya kisiwani ambapo walipewa refer kwenda muhimbili ambapo mtoto aliwekwa kwenye chupa lakini aliweza kuishi kwa siku moja tu na kikafariki jana na mama anaendelea vizuri tu

wakuu haya ni maelezo yangu ila kama mtapata nafasi ya kumhoji mama na baba mtoto wao ndio maelezo mazito zaidi na yenye kuumiza kwa yeyote anayeweza kutoa msaada wa kisheria anipm nimpeleke akafanye mahojiano ya kina wahanga
n.b manesi wa kigamboni na wale wa muhimbili wamesema kama kilifonyika ni complete abortion
 
Back
Top Bottom