PostGE2025 Msaada muhimu zaidi kuliko yote unaohitajiwa na waTanzania

PostGE2025 Msaada muhimu zaidi kuliko yote unaohitajiwa na waTanzania

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Kalamu

Platinum Member
Joined
Nov 26, 2006
Posts
22,898
Reaction score
33,309
Wakati tunawashukuru wote waliosimama na kupaza sauti zao juu kuhusu mauaji ya waTanzania waliouliwa kikatili sana wakitafuta HAKI mbalimbali za msingi mwezi Oktoba 2025; ni wakati sasa. kuwakumbusha kuwa kulaani mauaji hayo pekee haitoshi.

Tuwaombe, wakati juhudi zetu za kutafuta haki hizo zikiendelea; watuunge mkono kwa kuhakikisha kuwa Decemba 09, na kuendelea waelekeze macho na masikio yao kwa karibu zaidi kuangazia yote yatakayokuwa yakifanyika hapa nchini.

Wao wanao uwezo mkubwa wa kutazama na kuchunguza matukio yote maovu yatakayokuwa yamepangwa na hawa waliojitwalia madaraka kwa nguvu.

Tunaomba watupe msaada huo wa kutazama kwa karibu zaidi wahusika wote wa matukio yatakayoelekezwa kwenye kuwaumiza waTanzania wanaotafuta HAKI.

Watumie teknolojia zote walizo nazo kunasa matukio yoyote yanayolenga kuwafanyia uovu waTanzania..

Kazi ya kupambana na hawa waovu tutaitekeleza wenyewe.

Wasisubiri kuweka vikwazo au mazuio kwa wahusika baada ya kufanya maovu. Zuio muhimu ni kuwabana wasiendelee kuleta uharibifu.
 
Mungu atakuwa upande wetu. Hii game itaisha mapema sana sana
 
Back
Top Bottom