Msaada, mwanamke anatapika damu iliyoganda

Heavy equipment

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
1,456
Reaction score
1,005
Habari
Jamani nilikuwa naomba kuelimishwa nini tatizo la kutapika damu iliyoganda.
Kazi zake za kila siku anafanya kama kawaida na hakuna maumivu yoyote anayosikia ila ikifikia wakati wowote anatapika damu iliyoganda, naombeni mnijuze mnaoelewa hili tatizo.
Ahsanteni
 
Hii inaitwa upper gastrointestinal bleeding ( Upper GI bleeding ) na hii ni emergency wala hihitaji kuja hapa kuomba ushauri bali mkimbize hospital afanyiwe matibabu ya haraka. Hii inawezekana ikawa ni esophageal varices, ambayo sababu yake hutokana na shida kwenye ini yaani Liver cirrhosis. Lakini pia inawezekana ikawa ni vidonda vya tumbo ingawa angekuwa na maumivu ya tumbo ya mara kwa mara. Kikubwa nenda hospital kubwa afanyiwe vipimo
 
Matumizi mabaya ya teknolojia ya habar na mawasiliano haya-sasa si umpeleke hospitali unakuja kuomba ushauri tena?bila kusema labda umempeleka hospitali mara kadhaa imeshindikana!!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…