Msaada: Mwanamke hajafunga ndoa na Mumewe ila wameishi wote na kuchuma mali kabla mumewe kufariki. Ni sawa watoto wa nje kumtaka auze nyumba anayokaa?

Msaada: Mwanamke hajafunga ndoa na Mumewe ila wameishi wote na kuchuma mali kabla mumewe kufariki. Ni sawa watoto wa nje kumtaka auze nyumba anayokaa?

netti mimi

Senior Member
Joined
Oct 10, 2016
Posts
147
Reaction score
109
Habari wakuu,

Naomba kuuliza kuhusu hii sheria. Kuna mama angu mdogo amezaa mtoto moja na mumewe ambaye mumewe kwa sasa kafariki huku ameacha watoto wa nje watatu.

Sasa shida ni wale watoto, walikuwa wanamsumbua huyu mama auze nyumba mpaka kwenye Kata. Huyu mama hakutaka, akaa mpaka sasa ameamua kuuza nyumba kwa hiyari yake ili awape awa watoto wa nje ili usumbufu uishe na kila mtu ale hamsini zake. Cha ajabu sasa hivi wanakataa.

Na huyu mama kutokana na usumbufu, anataka kuuza aondoke. Wanadai eti, anauza kwa bei ndogo. Thamani ya nyumba hawaijui, wao ni kulalamika tu.

Je, huyu mama akiamua kuuza yeye mwenyewe kunakosa? Maana anawaita hawataki. Na je, afanyaje? Au auze na fedha apeleke Serekali ya Mtaa? Mama ni mdogo hajafunga ndoa na huyu mwanaume, ila wamechuma wote mali.

Naombeni majibu wakuu.
 
Back
Top Bottom