Phdum
JF-Expert Member
- Apr 15, 2019
- 1,322
- 3,278
Habari zenu wana jf?
Ni mwezi sasa toka mama watoto wangu ajifungue lakini toka alivyojifungua alikuwa na tatizo la maziwa kuwa machache. Na tukafanya kila mbinu ili mziwa yaongezeke ikiwa ni pamoja na kumuwekea ratiba ya kunywa supu ya makongoro, kula ugali wa dona pamoja na kumtengenezea uji wa lishe bila kusahau pilipili manga kwenye uji na supu kwa sana.
Baada ya kufanya hivyo kidgo maziwa yalianza kutoka lakini sio katika kiwango kinachoridhisha, kwani mwanangu ana mwezi na wiki zake lakini afya yake kama ana wiki 2, Naombeni ushauri kwa wale wazoefu pamoja na ma dr wa hapa kama naweza nikamuanzishia mwanangu chakula mbadala kwa umri wake huo wa mwezi moja, au labda kama kuna namna nyingine ya kumfanya mama ake apate maziwa mengi na yakutosha.
Kwani kwa ma dr niliowaona wananiambia akazanie tu pilipili manga wakati mwanangu ukuaji wake ni wa kusuasua. Naomba kuwasilisha.
Updates.
Wana jf poleni na majukumu yenu ya kila siku.
Nimerudi tena kuleta mrejesho kuhusu andiko langu hapo juu, kwani nilijaribu kutumia mbinu na njia nilizoelekezwa na wadau, lakini naweza kusema kuwa njia moja tu ndio niliweza njia yenyewe ni kumpa mwanangu maziwa ya kopo.
Kulingana na mzingira ninayoishi maziwa yanayopatikana kwa urahisi ni lactogen na infacare hivyo nilimchukulia ya lactogen.
Lakini kwa masikitiko makubwa nasikitika na namwonea mwanangu huruma, kwani SITOWEZA TENA KUMUDU GHARAMA ZA MAZIWA YA KOPO. NA NATEGEMEA KUMUANZISHIA MAZIWA YA NG'OMBE NA KUMKOROGEA UJI MWEPESI (n.b mwanangu ana miezi 2).
Kwanini nimefikia hatua hii? Kusema ukweli najiskia vibaya sana ila kwa hali yangu kiuchumi imebidi nichukua maamuzi haya, kwani maziwa ya kopo ni tsh elf 25 na mwanangu anatumia ndani ya siku 2 siku ya 3 amemaliza kopo moja na hapo na maziwa ya mama pia ananyonya japo sio mengi na kijana mwenzenu sina ajira rasmi napambana tu mtaani kwa kweli hali ni mbaya, na mzunguko wa biashara umekuwa mdogo sana. Mwanangu nakupenda sana ila sina budi kukulisha uji kwa umri wako huo.
Pia nilijaribu kuwashauri baadhi ya wataalam wakaniambia maziwa sio mazuri kwa umri huo lakn nitafanyaje? Nimuache mwanangu akonde? Au alie usiku kucha kwa kutoshiba? Dah Japo nimeambiwa mwanangu hutokuwa na akili kwa aina ya vyakula unavyokula kwenye uchanga wako ila naamini Mungu atakusimamia tu na utakuwa na akili tu.