Msaada mwanangu hataki kulala

Tony Gwanco

JF-Expert Member
Joined
Jan 22, 2013
Posts
5,913
Reaction score
1,215
Salaam wana JF.

Poleni na majukumu kama kichwa cha uzi kinavyo someka.

Nina mtoto mwenye umri wa mwaka na miezi minne hapati usingizi ikifika saa nne za usiku ndio michezo inazidi na anataka kampani mwanzoni tulihisi ni kawaida ila siku zivyosonga anaonekana tabia imekomaa

Mimi na wife wote huamkia kazini na kurejea home jioni tukifika ndio kama amewekewe ufunguo ni michezo hadi saa saba hata ufanyeje ukimzuia ni kulii tukiuliza kama amelala mchana wanajibu kalala kidogo

sasa naona hadi mwili umeanza kupungua .nishaulini wanye uzoefu wa hili au lililo wahi kuwatokea

Thanks in advance
 
Pole sana. Mwanangu ana miaka mitatu na miezi nne sasa. Naye ana tatizo kama hilo la kukosa usingizi. Ilitusumbua kiasi. Jambo moja nililogundua ni kuwa hapati michezo mingi ya kumfanya achoke. Niligundua hivyo kwasababu ilikua tukienda kijijini ambapo anahangaika kutwa nzima (kuchunga, kulima, kuchota maji, kukimbiza kuku, na kila aina ya mchezo) basi atalala mchana na usiku mapema tu analala. Sasa huku mjini anachezea sebuleni tu, atachokaje? atapataje usingizi?

Nawashauri muongezeeni michezo (vifaa vya kuchezea na kumweka busy zaidi. Ale kwa ratiba inayoeleweka na kwa kiasi fulani ratiba ya kulala iwepo na izingatiwe sana. Pia mkamuone mtaalamu wa watoto atawashauri vyema zaidi.
 
Nikweli kabisa mtoto asipochoka hawezi kulala, mie kabinti kangu kana miezi sita lakini hizo shughuli zake hatari akilala sasa hadi mnasahau. Mwongezee michezo pia muone daktari wa watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…