Msaada: Mwanaume ninayeishi naye haoneshi kunipenda na hataki tuachane

Hahahahha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka juzi

Mwaka jana

Safari ilianza kitambo
 
Huyo Jamaa yako ni kauzu.amekomaa kihisia na ni mzito wa kuonesha hisia zake.Cha kufanya.Tuliza kiranga umri umeenda huo kwanza una bahati kukuta akiwa hivo.Huyo atakuja kuoa mke wa pili ili kukuacha hilo sahau kabisa.Kubaliana na hilo
 
Tafta Kitabu 5 love languages..
Yawezekana...yaonekana anakupenda kweli na we unampenda ila lugha yenu ya kuonyesha mapenzi iko tofauti...

Wewe labda kufanyiwa vitu vizuri kujuliwa hali ndo unapenda zaidi...yeye labda anapenda zaidi kushikwa shikwa esp kwny mchezo na maneno mazuri

Ili mapenzi yaendelee inabidi kumuonyesha mapenzi kwa style anayoelewa yeye...upo nyonyoo?

Na wewe mwambie vile vitu unapenda ili akufanyie...mapenzi yanajengwa hayatokei tuu
 
Mkuu si ungeandika tu kiswahili?
[emoji23][emoji23]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa umeolewa na msukuma halafu unataka uitwe sweet, baby, asali, laazeez, elhabeeb, na majina mengine romantic??

Tangu lini wasukuma watu washamba Tanzania hii wakawa romantic??

Anakupenda ila naturally wasukuma hawajui hayo mambo ya kupetipeti hususani kama huyo mumeo alokulia huko Magu mchunga ngo'ombe huyo!
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila dada punguza kuwa na expectations kubwa, huyo jamaa anakupenda, sema tu hajui jinsi ya kuuonesha upendo wake kwako. Hivyo basi, tumia nguvu ya kike kumbadilisha. Haya mambo ya birthday wengine huwa hatufagilii, ni asili na malezi yetu.
Na hicho kipato cha mshikaji mbona cha kawaida sana, maana hiyo figure uliyoitaja ukitoa makorokocho ya bodi ya mkopo, income tax, na mifuko ya jamii hapo unakuta anachukua 1.3, ambazo hata kuhonga michepuko hazitoshi [emoji23][emoji23][emoji23].
Tulia myajenge maisha, na jaribu kuongea naye, ukiongea nje nje hatajua.
Mambo mazuri hayataki haraka, na kama unataka kufungua biashara si unamshirikisha with a detailed plan na estimate ya gharama na umuhimu wa wewe kuwa na kazi . Hakuna mwanaume mwenye akili timamu anaweza kukataa.
Ukiachana na naye unaweza kutana na makubwa huku nje, kuna mwenzio anakuta KY na Condom kwenye gari kila siku( and possibly anakuwaga posted instagram my lovely wife na birthday party ya maana tu)
Na kingine nilichokinote jamaa yako hana financial skills( hajui kumanage kipato chake) Ila hilo linafundishika.
# ukiishi na hizo doubts hamtafika mbali.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
KUNA ISSUE NYING SANA HAPA!!

but kubwa kuliko yote is
HAUNA FURAHA NA HAYA MAHUSIANO!!

amua kuendelea at your risk!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…