X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,400
- 14,339
Nimekaa nikafikilia maisha yamenipiga, kazi niliyokuwa nayo haikidhi kabisa mahitaji yangu ya kila siku, nina mke, nina mtoto, ninao ndugu wanao nitegemea, baba, mama na wadogo zangu mbaya zaidi mimi ndie kaka mkubwa wa familia, najiona kabisa nimeanguka, najiona napoteza uelekeo kila kukicha, nimekuja humu najua kuna watu wa hadhi na kariba tofauti tofauti, maana waswahili husema "mficha maradhi kifo humuumbua"
Nimehangaika kutafuta kazi, ni kweli nipo kwenye kazi ambayo mshahala ni 250k baada ya makato, huo mshahala unanifanya niishi kwa madeni hata kabla sijaupokea unakuwa teyari umeshaisha, sasa ndugu zangu kwa umri wangu huu 25+ najiona kabisa ndoto zangu hazitotimia, nikiwa na akili timamu ninaomba kwa yeyote mwenye connection ya ajira, ata ya ULinzi, na nyinginezo kwenye nchi za kiarabu haswa Doha, Qatar anisaidie pengine huko maslahi yanaweza kuongezeka.
Nimejaribu kufuatilia kwenye mitandao nakutana na maagency ambao wapo nchi za jirani inakuwa ngumu kwangu kuwafikia kwani wengi wao wapo Kenya ama Uganda.
Ndugu zanguni ni matumaini yangu kilio changu kiapatiwa ufumbuzi.
Elimu yangu ni ya kidato cha nne, sijasoma kihivyo ila ujinga wa kuelewa kingereza kidogo nimeuondoa hivyo ninaweza kingereza japo si sana.
VILE VILE mimi ni dereva wa magari...mwenye leseni yenye daraja A, A2, B, C1, C2, C3, D, E

ANGALIZO
lengo la huu uzi lilikuwa kupeanda connection za ajira nje ya nchi lakini kumejitokeza watu ambao sio waamini wanao onyesha nia ya kumsaidia mtu kumbe lengo ni kufanya utapeli.
usitoe pesa kwa mtu usie mfahamu japo ni kweli kuwa kwa asilimia 75 kampuni nyingi ni lazima ulipie gharama ili wakusaidie.
kabla hujatoa pesa kuna wakala wa serikali anae jihusisha na maswala ya ajira kampuni zote hizo zipo chini ya kitengo hicho.
hivyo ni bora kwanza ukaenda kujiridhisha TAESA kuhusu kampuni inato taka kukufanyia mpango wa safari.
huyo mtu hapo juu ambae ni member mwenye jina kubwa tu humu JAMIIFORUMS alitaka kunitapeli nisingekuwa najua michongo ya mataperi hivi sasa Ningekuwa nalia.
usitoe pesa bila kuwa na uhakika wa ajira. viza kwanza pesa baadae msije kusema siku waambia...!