Unataka umama ntilie wa aje kufungua mgahawa au kutembeza? Au plan ni kuuza uzaje.... Hii ya kutembeza naona ni nzuri zaidi
Ukianza na mahesabu ya hadi ununue ma viti mafriji hautoboi, labda kama huo mtaji upo.
Hii biashara mi nilifanyaga enzi hizo nikiwa naishi home, mtaji ni masufuria ya maza 😁. Kuna mdada alikua anauza juice pale mtaani ndo nilimuomba lift akipeleka juice ananipelekea na msosi.
Napika wali, maharage, nyama na mboga za majani tuu...PIKA CHAKULA KIZURI wateja hawaondoki. Na ujiboreshe nunua visahani vizuri hata kama ni cha mfupa ila kizuri sio ile misahani ya mabati
Jitahidi sana uwe msafi, ukishapika kimbia oga ndio uanze kuuza usizunguke zunguke na jasho lenye mixa ya nyanya na vitunguu
Hebu ingia field zungukia humo kwa hao kina mama angalia wanavofanya anza biashara na kidogo ulichonacho, usiombe ombe sana ushauri wa watu UTAKWAMA