Msaada: Nahisi kuishiwa mbinu

Lol................

Cha muhimu ukikutana naye mwoneshe kuwa unamwitaji, chukua mawasiliano yake, usiwe unampigia daily, atakuchoka.
kisha kama anaweka pozi mpotezee, nikiwa na maana ya kupunguza au kutata mawasiliano kulingana na jinsi anavyokuchukulia..
Ukimpotezea (kukata/kupunguza mawasiliano naye) usijenge bifu, wala usiwe unamkwepa pindi ikitokea mkakutana barabarani
Msalimie, mwoneshe uchangamfu wote, ila usizidishe. kama yuko interested atakuuliza mbona umekuwa kimya,
jifanye kuna maswala yamekufanya uwe bize, kisha mpe ahadi kuwa utampigia jioni au kesho yake..
Usimpigie kama ulivyo muahidi, hapa ataweza kupiga yeye akiona umekaa kimya sana.
Kama hayuko interested hatokuuliza kuhusu kupotea kwako. Hivyo achana naye.
kwenye simu usiongelee kabisa kuhusu kumtaka bali jadiliana naye mambo mengine tofauti...
Mcheki jinsi atakavyokuwa ana-react..
endelea hivyo mpaka pale utakapofanikiwa lengo lako..
Cha muhimu kuzingatia, hata siku moja usimuoneshe kumchukia au kukerwa na jinsi anavyokuchukulia kama hakutaki,
Usimnunie binti anayekupiga kibuti, utampa kichwa zaidi..


Hii mbinu inaweza isi-work kwako, ila jaribu... Kwangu inafanya kazi vizuri tu.
 
me nadhani bado hujampata anaekupenda kwa dhati,akija huyu hata iweje lazima awe wako.
 
thanx kwa maelezo mazuri, nitayafanyia kazi
 
Nakumbuka kipindi kile nikiwa form 5 nilianza kukafuatilia ka demu flani hivi almost 8 month so kwakuwa kalikuwa kanapenda kusoma na kalikuwa kamefaulu ili nibidi niwe na kapiga saund alafu kakikimbilia kwenye issue za shule bac hapo ndo najidai ndo mshauri haswa ikafika mahali kidogo kaingie laini! Lol! Baada ya miezi 9 kupita kakaja kaka nijibu 'soma kwanza'' bas nikaamua kukapotezea heh! Kumbe kaongo baadae kakaanza kunitafuta but hadi leo sijawah kurespond Anywaz Msichana kama anakupenda baada ya kukuzingua ukichuna mwenyewe ataanza kukutafuta.
 
Poyeeeee tindikali, jitahidi buni mbinu mpya, sie wanawake tunaangalia vitu vingi sana kama ulivyoambiwa, kwa mfano mimi mwanaume ambaye viatu vyake/miguu yake vi/inanuka hata awe wa namna gani siwez kumkubali!! nahisi kichefu chefu tu.....so jiangalie sana kwani kila aspect yake hata kama iwe ndogo vipi ina sehemu katika kuboresha penzi lako
 

thanx mrembo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…