Msaada; Nahitaji kununua Samsung. Je, version gani ni current na ipo vizuri?

Sim inauzwaje sumsang A35
 
Ni low end. Ni simu ya kawaida sana. Haiko tofauti sana na simu nyingine za bei hiyo
Kamera yake pia ni ya kawaida sana. Inatunza chaji, design nzuri, kwa bei yake kioo ni kizuri pia ila nothing too shocking
Nikienda kariakoo naweza kuipata?.
 
Ni low end. Ni simu ya kawaida sana. Haiko tofauti sana na simu nyingine za bei hiyo
Kamera yake pia ni ya kawaida sana. Inatunza chaji, design nzuri, kwa bei yake kioo ni kizuri pia ila nothing too shocking
Mkuu Xiaomi ya bei sawa na samsung A35 inakuwa na sifa gani za ziada ukilinganisha na samsung?
 
Mkuu Xiaomi ya bei sawa na samsung A35 inakuwa na sifa gani za ziada ukilinganisha na samsung?
Redmi Note 14 Pro 5G ndio bei sawa na hiyo Galaxy A35

Kwa hapa Mbeya, duka la Mtawa Enterprises inauzwa laki 7 kwa version ya 8GB RAM 256GB ROM

*Ina kamera nzuri kuliko A35 overall
*Inachaji faster kuliko A35 (45W vs 25W)
*Inakuja na IR Blaster (A35 haina)
*Inakuja na Reverse Charging feature (A35 haina)
*Ina kioo kizuri zaidi ya A35, kina mwanga angavu zaidi juani kuliko A35 (1138nits vs 1020nits) ni cheusi na kiko sharp kuliko cha A35 huku pixel density yake ikiwa 446ppi (Galaxy A35 ina 390ppi)
*Ina Bluetooth version mpya zaidi (v5.4 Vs v5.3)
*Kioo cha Redmi Note 14Pro kina Dolby Vision na protection ya juu kuliko A35 namaanisha glass ya juu kabisa kwenye kioo. Hii Redmi ina Gorilla Glass Victus 2 wakati A35 ina Gorilla Glass Victus tu ya kawaida yani ya version ya kwanza
*Frame ya Redmi Note 14 Pro 5G imetengenezwa na metal, ila ya kwenye A35 ni plastic
*Processor ya Redmi Note 14 Pro 5G ni nzuri (4nm) kuliko ya kwenye A35 (5nm) ingawa utofauti sio mkubwa
*Battery ya Redmi Note 14 Pro ni Lithium Polymer (Li-Po), ni nzuri kuliko Lithium-Ion battery ya kwenye A35 (Li-I)
*Kwenye boksi la Redmi Note 14 Pro 5G unakuta charger, kwenye A35 hukuti inabidi ununue mwenyewe

Na overall Redmi Note 14 Pro 5G ni simu nzuri kuliko Samsung Galaxy A35
 
Sijui nihamie REDMI nitest na huko maana nimetumia Samsung muda mrefu.Hivi hazina mambo ya kustack?
 
Nashukuru sana mkuu Reuben Challe
Lengo langu ni kuinunua Xiaomi (Redmi Note 14 Pro) baada ya kunishawishi kama hivi.
Naomba nijue pia namna ya kuithibitisha kuwa sio fake ili nisisumbuke sana kuzunguka maduka na kutafuta huruma ya wauzaji ambao wengi sio wakweli. Ningekuwa Mbeya ningekuja kwenye duka tajwa ila kwa sasa niko Dar.

Natanguliza shukrani mkuu.
 
Kuna njia mbalimbali za kujua kama Xiaomi yako ni fake au original

1. KUHAKIKI IMEI NUMBER
Chukua simu yako ingia kwenye Call App halafu dial *#06# then utaona IMEI number za simu yako. Mara nyingi simu za Xiaomi huwa zinakaa laini mbili kwa hiyo IMEI number zitakuja mbili. Ziangalie kama hizo IMEI number zinafanana na zile zilizoandikwa kwenye boksi la simu yako
Kama zinafanana basi simu yako ni ORIGINAL

2. KUHAKIKI MODEL NUMBER
Njia nyingine ni kuhakiki Model number. Kwenye Xiaomi, ingia Settings, nenda About phone, chagua "Detail Info and Specs" then zitakuja specifications za simu yako. Shuka hadi walipoandika model number. Copy hiyo Model Number pembeni
Ingia Google kwenye sehemu ya ku search iandike hiyo model number halafu search uone kama simu itakayokuja ndio hiyo Redmi unayotaka kununua. Kama ukiingiza model number za Redmi Note 14 Pro then ukigoogle itakuletea Redmi Note 14 Pro maana yake ni ORIGINAL

Au angalia kama model number ya kwenye simu inafanana na iliyoandikwa kwenye boksi la simu. Inabidi zifanane

3. KUHAKIKI UBORA WA SIMU
Unaenda kununua Redmi Note 14 Pro maana yake unajua ina kioo kizuri cheusi angavu, kamera nzuri, unajua design yake, na sifa zake nyingine kwa hiyo unaponunua iangalie simu yako hakikisha kweli ina kamera nzuri, kioo kizuri cheusi na ang'avu, design ileile na sifa nyingine unazozijua
Kama simu ina sifa tofauti na hizo basi sio ORIGINAL
More information on Redmi Note 14 Pro unaweza kuingia gsmarena pia
 
Sijui nihamie REDMI nitest na huko maana nimetumia Samsung muda mrefu.Hivi hazina mambo ya kustack?
Hapana. Redmi zipo faster, hazistack ovyo
Cha msingi nunua Redmi nzuri, maana Redmi zipo hadi za chini kama "Redmi A5" ambazo sio nzuri
Yani kwa Samsung ni kama vile uende kununua "Samsung Galaxy A03 Core", hauta enjoy uzuri wa Samsung: ndio kama hiyo Redmi A5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…