Msaada: Nahitaji kutengeneza 15,000 Tsh kwa siku

Msaada: Nahitaji kutengeneza 15,000 Tsh kwa siku

Kama wewe sio mtu mzima sana ni bado kijana flani mchangamfu fanya hivi.
Chukua hiyo laki moja nenda kkoo maduka ya vitenge unaomba kuiweka rehani hapo kisha unapewa vitenge vipya pc 4 unazotundika mabegani unaingia nazo changanyikeni mitaa hiyo hiyo ya soko kuwasaka wateja hasa wageni, unawakaribisha dukani ulipochukua vitenge.
Ukiwapata wawili watatu kwa siku wanakutosha.
Pale dukani kila mteja utakaempeleka kila kitenge atachochukua unapewa buku 1 so unaweza pata hata hiyo 15 elfu hata mpaka laki kwa siku inategemea na bahati na uchakatikaji wako.
Unawajua wauza maduka kkoo wewe, uwape laki 4 yako uiweke rehani alafu utegemee wakurudishie nawakati wanamadeni bank madeni yamizigo ya mabosi, wachache Sana Kati ya kumi labda mmoja
 
Hahaha forex ni biashara ya msimu? Hahaha jamaa yangu unachekesha kinoma🤣🤣🤣🤣🤣
Ukiielewa Sana Forex huwezi kucheka sana anaposema biashara ya msimu.

1. Kwanza out of 7 days kuna Siku 4 Tu ambazo ni active for trading.

2. Kingine miezi ya June hadi August na mid December to mid January soko huenda kibla

Kwa haraka haráka active trading months ni kama 8 Tu afu Katika kila mwezi una siku 16 za kutrade actively na uombe pawe na volatility.

Ukilazimisha kutrade choppy au side ways markets ilimradi uonekane unafanya biashara mda wote utapoteza hela nyingi sana
 
angalia unapokaa mtaani au sehemu hyo unayoishi kuna nini kinakosekan alfu kinahitajika kwa sana au kitu au huduma utakayo ileta watu watakayo ipenda au kuinunua kiulaini

1 Kama ni nafaka mchele mahindi ww zama kijijini chukua mzgo

,2 au mavazi nguo au viatu vkali sana pea ata 5, ingia kariakoo chukua bidhaa ambayo ata kama mtu asipo nunua ataitazama mara mbilimbili

3 Kama kuna xhida ya kuku, bata , au mayai zama vijijini ndannindani chukua mzgo

4 Au anza biashara ya matunda nunua matunda ndiz, iparachichi, embe nk
Tafta ndoo , maji safi sahani kadhaa kakabati ka kiaina , benchi na location ambay watu hukutana san mfano bus stop au mbele y hotel ambap watu weng huend au kijiweni. anza kuuza matunda , ww unakat mtu anakaa kweny benchi anakul kweny sahan akimaliz anasep
5 kama upepo wakutembez sambusa,mayai, ice cream, jojo na pipi, karanga ufut a anza kazi

6 au mcheki mtu alieanzsha biashar wekeza fedha au partnership mta gawana kitakacho patikana mfno kam ni y chips ila anash y fedha mkubaliane au mama ntilie au wauza soko ukubaliane mwaga pesa

Natzan utapta kitu apo.....
Hamna steshenari yani watu mpaka wavuke barabara
 
Na hili nalo mkalitizame

Naombeni mwongozo wa biashara yoyote halali ya kufanya kwa hapa Dar es salaam itakayoniwezesha kutengeneza 10k hadi 15k kwa siku.

Biashara iwe ya mtaji kati ya 100k na 200k na inayohitaji mazingira rafiki ya utendaji kazi, pia isiyo na changamoto nyingi

Nawasilisha
Hiyo 100 K nunuwa kanzu na kofia ,,birika tembeza kahawa ya alkasusu.

Hutojutia.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom