Waungwana najua humu kuna ma pharmacist na hata matabibu waliobobea na hata wagonjwa pia.
Hii dawa ya Gancyclovir ninaihitaji sana kwa ajili ya dada yangu ambae baada ya kufanyiwa endoscopy test kaandikiwa na specialist wa hospital kubwa hapo Dar.
Tumetafuta sana takriban pharmacy zote maarufu tumekosa Dar ni kubwa yawezekana kukawa na pharmacy ambayo dawa hii inapatikana na sisi hatukupita hapo.
Lakini pia kama Kenya , Uganda , Rwanda na sehemu yoyote dawa hii inapatikana please tusaidiane kufahamu maana Dr kasema ni hii tu ndio dawa inayohitajika kwa mgonjwa wangu.
Wasalam