Msaada: Naitaji kulima mpunga (saro), naitaji mawazo yenu

Msaada: Naitaji kulima mpunga (saro), naitaji mawazo yenu

Anotsitse

Member
Joined
Sep 18, 2017
Posts
5
Reaction score
4
Habari zenu humu jamvini,nina mtaji wa shilingi laki Saba ,pia Nina eneo la Eka tatu jirani Na mto wami Morogoro .Baada ya mfumuko wa bei ya mpunga nimehamasika kulima mpunga Aina ya Saro Eka mbili,tafadhali naomba MAWAZO yenu.
 
Hio mbegu INA toa mazao mengi sana huku kwetu unaweza kutoa hadi gunia 40 kwa hekari sasa tatizo bei yak ni ndogo kuliko mpunga wowote ule sababu INA Michele mbaya sana
 
Huku kukatua 50,000
Kuvuruga 50,000
Kupanda 50,000
Palizi 50,000
Kukodi 100,000
Kuvuna 100,000
Hapo mpunga upomkononi mwako
 
hata kama una ardhi tayari lakini kwa laki saba haitoshi:
je una mbegu za mpunga za kutosha ekari tatu?
je umeandaa pesa ya chakula kwako na wasaidizi wako?
je umeandaa pesa ya kulinda ndege?(kama wapo)
hivyo kwa ushauri wangu jaribu kukaa chini na kufikiria vitu vingi kabla ya kuanza ili usije ukafanya vitu vya kuwachekesha walionuna.
 
Panda kwa njia ya SRI.

Unatumia eka chache ila mavuno ni balaa.
 
Laki saba inatosha kwa eka moja tu. Usiwaze eka mbili hasa kama watarajia kupanda kitaalamu labda kama ni wa kurusharusha mbegu unaishia kuvuna gunia saba kwa eka
Sawa mkuu nashukuru Kwa ushauri.
 
Mkuu kwa laki saba,ukijibanaa kwel kweli unalima heka mbili
 
Back
Top Bottom