Msaada: Nakataliwa na kila Msichana

quantumQ

Senior Member
Joined
Dec 11, 2013
Posts
111
Reaction score
84
Nahitaji msichana wa kuwa na mahusiano nae ila sijui pa kuanzia. Sio kwamba sijui kutongoza ila naogopa kukataliwa. Muda mwingi wa maisha yangu nimeutumia kwenye masomo sana sasa baada ya kumaliza kidato cha sita ,uhitaji wa kuwa na msichana wa ku share nae feelings ndio ukawa mkubwa zaidi. Tatizo kila msichana nitakaye mfeel nikimuelezea anazingua. Nikaona nisiende direct bali ni anzishe friendship kwanza tufahamiane zaidi ,kwa kuwa niko kwenye movement sana kutokana na masomo basi nikiomba hata namba wanakataa.

Sasa hivi nimekuwa affected kisaikolojia kiasi kwamba na wa hate girls, kila mmoja naona atanikatalia. Nimestop kuongea nao na sina marafiki wa kike pia nilisoma kidato cha kwanza mpaka cha sita shule ya wavulana watupu. Sasa hivi nipo chuo mwaka wa pili nachukua engineering ila sijamueleza msichana yoyote ambaye namfeel kwa sababu i have a fear of rejection.

Huwa naumia sana wenzangu kila siku wanatembelewa na wapenzi wao room, wanatoka out weekend wana enjoy, wanapeana zawadi ila mi kwangu hiyo ni ndoto.

Sasa najiuliza kweni mimi nina kasoro gani kama money ipo, darasani nafanya vizuri tu na nina think on positive side of life.

Kwa sasa nina miaka 22 na hii hali ina affect my studies i just want somebody to remove my loneliness ,to share love and happiness, doing things together and to make me feel worthy living.

The greatest effect now is that i don't want to talk to girls for what they Have done for me. I am living hoping that one day a girl will come who understands me but time is running
Please guys help me.
Regards.
Thanx
 
Hilo dogo sana na ni rahisi kupita maelezo,kwanza inata kujiamini na usiwe upande wa kuvunjika moyo ,muhimu kwa vile upo sehemu ingine ,itakuwa ndio ize ,vizuri anza kuzoeana nao mpaka wamekuzoea ,hapo mazoea yakishakuwa hayana wasiwasi chagua target yako na katika mazungumzo mkiwa mpo wengi au yupo na wenzake jaribu kumuunga mkono katika vyanzo vyake vya habari anavyoanzisha au mazungumzoni wala usiwe unamtazama ,ila kitu kimoja mtupie macho ya kawaida yasio na ishara yeyote ila uyatulize kwenye uso wake na jitahidi iwe mnagongana macho ,usigande zaidi ya sekunde mbili ,endeleza hali hiyo mpaka nayeye aanze kuizoea ,hii itamjia automatic wakati mkigongana macho na pia kuwa karibu nae wakati wa mazungumzo ya pamoja na wenzake.

Endeleza mpaka akuzoee kivyake na ajione yupo salama kwani hujamgusia chochote upo katika kuchanganya chemico tu,Sasa anza kupandisha joto ,katika mazungumzo ya pamoja ikiwa mwenzake hayupo muulize yyeye kwa kumwita jina lake fulani fulani yupo wapi ,akikujibu (ni lazima akujibu) endeleza mazungumzo kwa kuliizia huyo mwenzake ,labda atakujibu sijamuona,muulize mbona hujamtafuta mwenzio ,pengine anaumwa yaani umzungumzishe japo dakika tatu inne ,nia yako ni kujenga mahusiano ya karibu zaidi ,pia ukishaongeza mahusiano hayo ,sasa anza kuchimba shimo hapa unaweza kumuuliza suala lolote lile ,mfano unaweza kumwambia nyumbani wanataka kujenga nyumba lakini hawajui kuipanga jiko lipo wapi ukumbi waweke wapi una idea yeyote ile ? Kama una kalatasi ni vizuri zaidi na pencel ila baada ya maneno mawili matatu kupita kama ana ushauri atakupa na ridhika na oneza kuwa amekupa ushauri mzuri. Jingine kama unatafuta stori ,unaweza kuona paka au kuku au bata au mbuzi au ng'ombe ,jidai kushtuka nae kwamba umeona kitu labda ukamwambia mtizame yule ,atakuuliza kwani ana nini ,utamwambia nyumbani mlikuwa nae kama yule ukimpenda kwelikweli lakini aligongwa na gari basi ametuhuzunisha sana nyumbani ,unaona eei ,kisha unamgeuzia yeye suali hilo kwani wewe mnapenda nini ,usitumie unapenda nini ,tumia mnapenda nini .nyumbani kwenu au mna mifugo ,hapa unatafuta kuuteka moyo wake na kudumisha ajione yupo na mtu anaejali,hii inakuwa ndani ya moyo wake,hivyo ukifanikiwa kwa hayo atakuwa kwanza hawezi kukukosa kukuona ,kumbuka hujamtajia kitu kuhusu mapendo ,saaaaaaaaasa ukishaona kazoea ,jaribu kumpima ,kivipi ? Anapokuwa na wenzake penda kuzungumza na wenzake na sasa usimtazame tena ,cheka nao changamka nao zaid hao wengine katika mazungumzo ya kawaida tu ,kama ameanza kukupenda atanyamaza kimya atakuwa hasemi na anaweza kuondoka hapo kwani utakuwa unajua kinachoendelea.
 
Pole mkuu,jiamini...ila miaka22 bado mdogo,zingatia masomo kwanza,usibabaike ukiwaona wenzio na wapenzi, mapenzi ya chuo huwa hayadumu!na siku hizi magonjwa nje nje hujui mungu anakuepusha na nini?!
 
Mbona muda bado sana? Halafu mapenzi ni zaidi ya pesa, kufanya vizuri darasani na 'kuthink positive' mapenzi hayana formula
Epuka kuwa too much defensive, usijitenge nao utaonekana unaringa au unajipa daraja fulani katika maisha, usiwe serious sana jichanganye na jaribu kuwa mcheshi kwa kiwango chako utaona greelights kibao

Bado hujatendwa wewe kwakuwa bado huna mpenzi,jiandae yatakuja kukutokea na maumivu yake yatakuwa mabaya zaidi kuliko haya ya sasa
 
Pole mkuu,jiamini...ila miaka22 bado mdogo,zingatia masomo kwanza,usibabaike ukiwaona wenzio na wapenzi, mapenzi ya chuo huwa hayadumu!na siku hizi magonjwa nje nje hujui mungu anakuepusha na nini?!

Jestina acha dogo aanze kuwagonga mapema, si unaona wenzake wanagonga. Akilemaa akasubiri baadae atajikuta anachukua masazo yalioachwa na wenzake, hivyo yeye atakuwa ni loser. Umri huo alionao ndio mzuri kuanza kumuandaa mwenza wa maisha.
 
Nyege mshindo zinakusumbua kijana...

Hebu tia juhudi kwenye masomo kwanza hawa wanawake wapo tu kibao...
 
Umri huo alionao ndio mzuri kuanza kumuandaa mwenza wa maisha.

Anamwandaa mwenza wa maisha yapi hayo wakati maisha yake binafsi bado hajayaandaa???
 
uzinzi ni dhambi.soma wanawake wengi sana.ila sio lazima awe mwanachuo
 
pole jaribu kutongoza aina mbali mbali za wasichana ili ujue tofauti zao afu jiamini mademu wameumbwa kwa ajiri yetu
 
Pole sana mkuu,una tatizo kama langu tu yaani nachukia wanaume hadi nataman kuwapiga risasi wafe wote but its impossible ni ngumu ku handle.
 
Mapenzi na shule ni kama mrenda na pilau.

Matokeo ya mapenzi kwako sasa yatakuwa ivi..
G.P.A=pass, Msuli tembe matokeo sisimizi, Supp tatu au nne=Disco.

Mapenzi yanachukua asilimia kubwa sana ya mawazo yako kiasi kwamba yataathiri masomo yako, labda ungekuwa ulianza toka ukiwa form nyoya.

Achana nayo vumilia, ukiwa engineer hautakaa utongoze, wanakujaga wenyewe tu mkuu, hawa viumbe wadhaifu sana.
 


Bro mbona unamtisha sasa?
 
quantumQ wewe una inferiority complex, hilo ndio tatizo kubwa, huumii kwa sababu wasichana wanakukutaa ila ni kwa sababu unawaona vijana wenzako wakiponda nao raha, kutembelewa hostel nk. hivyo na wewe unahitaji kuwa kama wao, na inavyoonekana kama hao wenzako wangekuwa kama wewe usingejisikia vibaya, wala kuwahisi vibaya mabinti. wavuta bangi, unga, sigara na vyapombe wote wanakuwaga na tabia kama yako yaani huwezi kuwa wewe kama wewe kwa watu ambao hujui walipata malezi gani na ktk mazingira gani.
 
Last edited by a moderator:
Fanya bidii kuhuzulia nyumba za ibada,na ongeza bidii kwenye masomo.
 
Jestina acha dogo aanze kuwagonga mapema, si unaona wenzake wanagonga. Akilemaa akasubiri baadae atajikuta anachukua masazo yalioachwa na wenzake, hivyo yeye atakuwa ni loser. Umri huo alionao ndio mzuri kuanza kumuandaa mwenza wa maisha.

Mkuu acha unampotosha dogo, wanawake kila siku wanazaliwa hana hata haja ya kubabaika. Zingatia masomo kwanza siku ukifeli chuo ndo utajuta kusoma chuo kikuu.
 
Hivi shule si bado hazijafungwa? kaa usome kwanza madem wa nini na umri huo si ndo maana wanakukataa.
 

U.malaya unakusumbua, piga nyeto itakutoa lonilesi. Mi nimesoma form 1 hadi 6 bila wanawake, nikasoma mzumbe BAF darasani wanaume 150 wanawake 20 baada ya hapo nikapata kazi department nzima hamna mwanamke! Ila sikuona shida! We ndo mzinzi kabisa! Nenda kona bar kaanzishe mahusiano so umesema hela IPO? Ama level 9 pale Kilimanjaro kempisky
 
He he he! Unahate girls.. tafuta suluhisho fasta.. usije ukawa mpunga bure kijana wa watu, mapenzi sio pesa wala kufanya vizuri darasani.. wanawake wanataka kukomaliwa..kijana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…