Mahitaji: Nyama, chumvi, Tangawizi, kitunguu saumu, vinegar, ajinomoto, soya sauce, mafuta ya kupikia.
Andaa nyama yako. Nyama nzuri kwa kuchoma ni salala ndogo{T-Bone}au sehemu ya kidari. Ikate vipande size unayohitaji. Chukua Tangawizi usagie kwenye nyama au usage pembeni kisha uikamulie maji yake kwenye nyama, weka mafuta ya kupikia kidogo ili viungo vichanganyike. Baada ya tangawizi waweza kuweka garlic. Kisha chukua Vinegar nyunyizia kiasi kidogo kutokana na wingi wa nyama, baada ya vinega chukua soya sauce unyunyizie nayo kiasi kidogo, ili kuongeza ladha zaidi waweza weka Ajinomoto kidogo then weka chumvi kiasi unachohitaji. Baada ya hapo changanya vizuri mchanganyiko huo kisha uache kwa muda kidogo ili nyama ilainike.ikishalainika sasa waweza kuiweka kwenye jiko lenye moto ambao sio mkali sana. Kaa karibu na jiko ili uwe unaigeuza nyama kadri itakavyokuwa inaiva.
Cc
watu8,
Heaven on Earth,
Mike McKee,
Nivea,
Maxence Melo.