Msaada namna ya kuandaa nyama choma

Msaada namna ya kuandaa nyama choma

Mahitaji: Nyama, chumvi, Tangawizi, kitunguu saumu, vinegar, ajinomoto, soya sauce, mafuta ya kupikia.




Andaa nyama yako. Nyama nzuri kwa kuchoma ni salala ndogo{T-Bone}au sehemu ya kidari. Ikate vipande size unayohitaji. Chukua Tangawizi usagie kwenye nyama au usage pembeni kisha uikamulie maji yake kwenye nyama, weka mafuta ya kupikia kidogo ili viungo vichanganyike. Baada ya tangawizi waweza kuweka garlic. Kisha chukua Vinegar nyunyizia kiasi kidogo kutokana na wingi wa nyama, baada ya vinega chukua soya sauce unyunyizie nayo kiasi kidogo, ili kuongeza ladha zaidi waweza weka Ajinomoto kidogo then weka chumvi kiasi unachohitaji. Baada ya hapo changanya vizuri mchanganyiko huo kisha uache kwa muda kidogo ili nyama ilainike.ikishalainika sasa waweza kuiweka kwenye jiko lenye moto ambao sio mkali sana. Kaa karibu na jiko ili uwe unaigeuza nyama kadri itakavyokuwa inaiva.

Cc watu8, Heaven on Earth, Mike McKee, Nivea, Maxence Melo.
kumbe ni ajinomoto nilijua majinamoto.. asante sana..
 
Last edited by a moderator:
Cjui mnatumia kilo ngapi ila ukitaka nyama iive vizur na ilainika vizuri andaa nyama stek .kata vipande vipana kidogo ila

kisha sagia tangawizi na ki2nguu swaum weka chumv na ndimu kisha weka pilipili manga ya unag na masala kidogo na nyunyiza pilipil ya unga kwambali.na kama unapapai kidogo sagia kwenye nyama.papai inafanya nyama iive kwa wepesi hadi ndani
Ukisha changanya na viungo acha viingie kamahata lisaa au mawili

Kisha choma kwa moto wa wastan acha ikake vizur naimani ikisha iva ladha utakayo ipate kwenye nyama hio hutajuta na unaweza maliza peke ako.jikon

Nashukuru sana...Jamani karibuni...kesho nitafanya majaribio
 
Wataalam habari za asubuhi; natamani nijue jinsi ya kukausha nyama iwe vizuri na ladha nzuri; naombeni maujanja
 
Wataalam habari za asubuhi; natamani nijue jinsi ya kukausha nyama iwe vizuri na ladha nzuri; naombeni maujanja

Kwanza kabisa unapaswa kufahamu ya kuwa nyama ya kukausha haipaswi kuoshwa. Pili nyama ya kukaushwa haitakiwi kukatwa vipande vidogo vidogo bali inatakiwa kukatwa katika mapande makubwa makubwa. Kabla ya kukausha nyama yako unaweza ku-marinate nyama yako kwa kutumia limao, vitunguu swaumu, tangawizi, pilipili manga, chumvi na binzari ili kuifanya nyama yako iweze kuwa na ladha na harufu nzuri na ya kuvutia.

Unaweza kukausha nyama yako kwa kutumia jiko la oven au hata la mkaa. Lakini kwa matokeo bora zaidi; nashauri utumie jiko la oven.
 
Kuna umuhimu wa kuanzisha Uzi wa kuzungumzia maswala yanayohusu Mapishi umu Jamii Forum
 
Nataka kuanzisha bihashara ya kuchoma mishikaki, nazidi okota vitu hapa
 
Back
Top Bottom