Msaada namna ya kufikisha malalamiko JWTZ

Barabarani ni Traffic Police, so ndiyo inatakiwa waje wapime....ila kama unataka kubeba dunia tafuta kambi ya karibu kaulize utaratibu wa kufidiwa.......
 
umgekuwa umeumizwa ningekushauri kitu lakini kama hujaumia tena dereva boda boda nakushauri tu acha yaishe
 
Muibukie tu huko huko kambini asiposomeshwa number endelea mbele, watumishi wengi waoga siku hizi haki haki tu
 
Kwa haya Mataifa fukara wa akili ambayo raia wake wamekubaliana na utawala usio wa kisheria na usio na demokrasia huwezi kupata haki yako hapo.Kuna gharama kubwa sana huwa inalipwa kimya kimya kila siku na wananchi kwa kukubali kuwa na Taifa kama hili.
 
....Ushauri tu: kama umetoka salaam na umepata hasara kidogo tu isiyohitaji malipo, wewe Mshukuru Mungu na Uendelee na Mihangaiko yako.
Karma itamfanyia Kazi.
Duniani sio lazima kila kitu Upambane!
 
Sasa km ujaumia unatafuta nin? Mshukuru Mungu kisha nenda dukani kanunue side mirrow na indicator ni buku 2 mbili tu uendelee na maisha.
 
Pole sana. Mtumishi wa JWTZ anatakiwa kuwa kuheshimu sheria za barabarani kama watumiaji wengine, ni haki yako kusikilizwa. Unaweza kwenda kutoa taarifa kwa Mkuu wa Kikosi cha Kanda pia. Kama hawakupi ushirikiano unaweza kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza. Mhe. Mongela atamuagiza Mkuu wa Idara ya MP atakusikiliza.
 
Pole kwa yaliyokukuta mwaka jana nilishuhudia Lori lao lililokuwa kwenye mwendo kasi na kuparamia haisi yenye abiria na kuua watu 6 na majeruhi mengi!! Walichofanya waliwabeba wakawapeleka hospital ya jirani, na kuondoka zao!!
 
umgekuwa umeumizwa ningekushauri kitu lakini kama hujaumia tena dereva boda boda nakushauri tu acha yaishe
Sio bodaboda mkuu, naitumia tu kuwahi kwenye kusaka tonge
 
Mkuu wangu,kama unaweza kutembea vizuri,hujaumia sana achana na hayo mambo,,ila kama utaona wanaokushaur sijui uende kwa mkuu wa mkoa sijui kambini nakuomba ukienda utuletee mrejesho
 
kwa kua kuingia kambini kwao ni ngumu maana watakuhoji na ukieleza shida zako wenzie wa getini watamlinda,nenda hapo pembeni ya mahakama pale bwalo la mgambo kuna viongozi wa kijeshi watakusaidia,ukienda traffic police wanaweza wakahisi usumbufu kumtafuta afisa wa Jeshi na wakakupotezea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…