mimi bado ninayo ya kitabu class E kipindi wanabadilisha mfumo nilikuwa nje ya nchi,je naweza saidiwa pia kupata ii mpya
Nenda TRA pia kumbuka Tin Number yako, na shs 40,000/= wataingiz hiyo Ti Number yako kisha watakuelekeza kwenda Trafic kwenye ofisi zao. Trafic watairuhuu kama haina shida. Then utakwenda tena TRA na kuprint karatasi ya kulipia bank hizo fedha. Kumbuka kuwa kwa sasa haina haja ya kujaza zile karatasi kamazamani, ila kwa sasa Daraja E wanainyofoa kama huna cheti cha NIT,auVETA. japo kwa ufupi ni hayo na sijajua uko wapi kwa sasa.
Kama leseni yako ni ya magumashi usiende, maana palepale polisi wapo
daraja B,D mkuu!
mimi bado ninayo ya kitabu class E kipindi wanabadilisha mfumo nilikuwa nje ya nchi,je naweza saidiwa pia kupata ii mpya
Mkuu nenda moja kwa moja ofisi za TRA kitengo kinachoshughulika na utoaji Leseni za kuendesha vyombo vya moto na 1.Leseni halisi iliyokwisha muda wake. 2.Cheti chako cha kuhitimu mafunzo ya kuendesha gari (Cheti halisi) 3.Namba yako ya mlipa kodi,kama huna nenda ofisi ya TRA inatolewa bure. 4.Shilling 40,000/= za malipo ambazo utapewa maelekezo na afisa wa TRA utalipia wapi.
Hapo hakuna Rushwa wala dalali nenda mwenyewe usimtume mtu wala asikuguse dalali wa aina yoyote, onana na afisa wa serikali.