Msaada namna ya kuhuisha (re-new) leseni ya udereva

Msaada namna ya kuhuisha (re-new) leseni ya udereva

Maelezo ya mdau yanajitosheleza kabisa, hizo ndio hatua za kufuata ili uweze kupata leseni mpya.

Pia usisahau kwenda na leseni ya zamani siku utakapoahidiwa kwenda kuchukua hiyo mpya, kuna mzee mmoja mwembamba ana elements za kikoloni mbaya, usipokuja nayo hata kama umeisahau mkoani, hautakabidhiwa leseni yako mpya, unless uwe na police loss report ikiwa umepoteza ya zamani.

Ahsante Mkuu kwa maelezo ya nyongeza.
Nasisitiza kuwa usimtume mtu/dalali, nadhani huyo afisi Mwenye elements za kikoloni kuna kitu kimesababisha kuwa hivyo.

Mi yalinikuta siku ya kwenda ku-renew niliambiwa nipeleke Cheti Halisi cha chuo nilichosoma udereva of course mi nina Leseni Daraja C3 baada ya kuleta Cheti hakukuwa na longolongo yoyote nilienda trafiki ku- verify nikarudi TRA kuchukuwa paying slip sikuombwa hata senti moja ya Rushwa.
 
Nenda TRA pia kumbuka Tin Number yako, na shs 40,000/= wataingiz hiyo Ti Numb,.......rint karatasi ya kulipia bank hizo fedha. Kumbuka kuwa kwa sasa haina haja ya kujaza zile karatasi kamazamani, ila kwa sasa Daraja E wanainyofoa kama huna cheti cha NIT,auVETA. japo kwa ufupi ni hayo na sijajua uko wapi kwa sasa.
Huu ni utaratibu wa kishenzi.

1.) Kwanini wao wenyewe wasiwasiliane na Traffic database moja kwa moja ili kujua Kama TIN no. haina tatizo? Hii kuzungushana ni kutengeneza mazingira ya rushwa na kupotezeana muda, ni ushenzi tu.

2.) Kwanini nisilipe papo hapo kwa Tigo Pesa pindi wanapokuwa wame-verify TIN namba yangu na kui-clear? Hii kuzungushana tena benki ni kupotezeana muda, ni ushenzi tu.

3.) Kwanini wasiprint new license papo hapo Kama walivyo fanya vitambulisho vya kura? Hii kusubirishana ni kupotezeana muda, ni ushenzi tu.
 
Hahaha , Eti Naweza Kuongeza Daraja Kabla Ya Miaka 3 Kama Inavyotakiwa???
 
Ikiwa una Daraja A,B & D fuata maelekezo ya mtebetini ila kama una daraja kubwa Zaidi kwa maana ya A,B,D,E,F & G ama C unatakiwa kuanzia kwa Vehicle Inspector akague Leseni yako kwanza ndipo upate notification kwa ya kwenda kulipia TRA na process nyingine kufuata. Ila gharama ni hiyo hiyo 40,000
 
Ikiwa una Daraja A,B & D fuata maelekezo ya mtebetini ila kama una daraja kubwa Zaidi kwa maana ya A,B,D,E,F & G ama C unatakiwa kuanzia kwa Vehicle Inspector akague Leseni yako kwanza ndipo upate notification kwa ya kwenda kulipia TRA na process nyingine kufuata. Ila gharama ni hiyo hiyo 40,000
Eti Unaweza Kuchukua Leseni Leo Baada Ya Siku 2 ama 3 Unaweza Ukafanya Mchakato Wa Kuongeza Daraja Ulikuwa Na B , D Ukaongeza C3 Na Kadhalika??? Msaada Pliz
 
Eti Unaweza Kuchukua Leseni Leo Baada Ya Siku 2 ama 3 Unaweza Ukafanya Mchakato Wa Kuongeza Daraja Ulikuwa Na B , D Ukaongeza C3 Na Kadhalika??? Msaada Pliz

Ni kutokuwa na mipango mizuri, yaani uchukue leseni leo ilihali una mpango wa kuongeza daraja baada ya siku mbili...Madaraja yote ya C kwa maana ya C3, C2, C1 & C yanaambatana na uthibitisho wa vyeti halali vya vyuo vya mafunzo ambapo wadau wa usalama barabarani huhusishwa.. kwa hivyo kuepusha mikanganyiko isiyokuwa na ulazima ni vyema kufuata tu taratibu.
 
Ni kutokuwa na mipango mizuri, yaani uchukue leseni leo ilihali una mpango wa kuongeza daraja baada ya siku mbili...Madaraja yote ya C kwa maana ya C3, C2, C1 & C yanaambatana na uthibitisho wa vyeti halali vya vyuo vya mafunzo ambapo wadau wa usalama barabarani huhusishwa.. kwa hivyo kuepusha mikanganyiko isiyokuwa na ulazima ni vyema kufuata tu taratibu.
Je Unaposomea Udereva Wa Awali , Unapopata Chet na Leseni Class D " Je Unaweza Kufanya Mpango Pale Kabla Ya Kupata Class D , Ukaongeza Madaraja Juu Kwa Juu Ili ikitoka Leseni Ije Na Daraja B D C3 A3 . Inawezekana???
 
Je Unaposomea Udereva Wa Awali , Unapopata Chet na Leseni Class D " Je Unaweza Kufanya Mpango Pale Kabla Ya Kupata Class D , Ukaongeza Madaraja Juu Kwa Juu Ili ikitoka Leseni Ije Na Daraja B D C3 A3 . Inawezekana???

Ni vizuri kwanza kutambua madaraja ya leseni kwa mfumo wa sasa kama ifuatavyo:-

A- Leseni ya kuendesha pikipiki lenye au lisilo na sidecar na ambao uwezo unazidi 125cc au 230kg.

A1 - Leseni ya kuendesha pikipiki lisilo na sidecar na ambao uwezo ni chini ya 125cc au 230kg.

A2 - Leseni kuendesha vyombo vya moto vyenye miguu mitatu au minne.

A3 - Leseni ya kuendesha pikipiki ambao uwezo wake hauzidi 50cc.

B - leseni ya kuendesha gari aina zote za magari isipokuwa pikipiki, magari ya biashara, magari yenye ujazo mkubwa na magari ya utumishi wa umma.

C - leseni ya kuendesha magari ya utumishi wa umma na yenye uwezo wa kubeba abiria 30 na zaidi kwa kuongeza dereva, Magari katika jamii hii inaweza kuwa pamoja na kuwa na kiwango cha juu yenye tela lisilopungua uzito wa zaidi ya 750kg. Waombaji lazima wawe na leseni ya daraja CI au E kwa kipindi cha si chini ya miaka mitatu.

C1 - leseni ya kuendesha magari ya utumishi wa umma na yenye uwezo wa kubeba abiria wasiopungua15 lakini wasizidi 30.

Abiria pamoja na dereva. Magari katika jamii hii yanaweza kuwa pamoja na kuwa na kiwango cha juu chenye tela lenye uzito usiopungua zaidi ya 750kg. Waombaji lazima wawe na leseni ya daraja D kwa kipindi cha si chini ya miaka mitatu.

C2 - Leseni ya kuendesha magari ya utumishi wa umma na yenye uwezo wa kubeba abiria si chini ya wanne na wasiozidi kumi na tano. Magari katika jamii hii yanaweza kuwa pamoja na kiwango cha juu chenye tela lenye uzito usiopungua zaidi ya 750kg. Waombaji lazima wawe na leseni la daraja D kwa kipindi cha si chini ya miaka mitatu.

C3 - Leseni ya kuendesha magari ya huduma za umma yenye uwezo wa kubeba abiria wanne au chini ya hapo, pamoja na dereva. Magari katika jamii hii yanaweza na kiwango cha juu cha tela lenye ujazo wa uzito usiozidi 750kg. Waombaji lazima wawe na leseni za daraja D kwa kipindi cha si chini ya miaka mitatu.

D - leseni ya kuendesha kila aina ya magari isipokuwa pikipiki, magari yenye ujazo mkubwa na magari ya utumishi wa umma.

E - leseni ya kuendesha kila aina ya magari isipokuwa pikipiki na magari ya mtumishi wa umma. Waombaji lazima wawe na leseni ya daraja D kwa kipindi cha si chini ya miaka mitatu.

F - leseni ya kuendesha magari makubwa yenye muunganiko wa matela.

G - leseni ya kuendesha magari ya shamba au ya kuchimbia.

H – leseni ya muda kwa madereva mwanafunzi

MUHIMU
Kabla ya kutoa leseni ya kuendesha gari kwa mtu binafsi, mhusika lazima kwanza awe amehudhuria mafunzo ya kuendesha gari na kuhitimu. Baada ya hapo atafanyiwa majaribio na kukabidhiwa tuzo ya leseni kulingana na daraja ambalo yeye aliomba na kufaulu. Kama dereva anataka kuendesha magari aina mbalimbali, anatakiwa kupitia mafunzo kwa ajili ya kuendesha makundi yote ya magari yenye leseni zilizoorodheshwa na akifaulu mtihani atazawadiwa leseni itakayoonyesha makundi ya daraja zote ambazo yeye amefaulu.
 
hiyo 40,000 ni hela ya serikali ila kuna watu wanajiita madalali kunajamaa juzi amepigwa hadi laki mbili na kumi,ili kuepuka usumbufu sijui uende kwa trafic we nenda na laki moja vinginevyo utasumbuliwa tu na huo usumbufu hauna maana nyingine zaidi ya rushwa tu.
Mkuu hayo huwa wanayataka wenyewe lakin taratibu zipo nahazina ugum mimimwenyewe imeisha lakini najua siwezi lipa zaidi ya 40 ila ninachojua kama unataka itoke sikuhiyohiyo unawatoa wale jamaa hata cha 5 anakuprintia leoleo.tunaita kujiongeza hahahahhaha laki mbili lesen ya ndege au?
 
Wadau kama ushapata leseni ya lena na ukaenda chuo ukapata cheti je taratibu za kupata leseni yenyewe zipoje?
 
Habari za humu, kuna rafiki yangu alipoteza leseni yake ya kuendeshea gari na anahisi amepotezea porini na kuipata itakua ngumu.
Je kuna gharama kwa ajili ya kupata leseni mpya? maana hiyo alirenew November 2017.
Na je ni gharama ni kiasi gani?
Asanteni
 
Nenda pale Mayfair plaza mikocheni ukiwa na leseni yako ya zamani, utapewa karatasi ya kulipia benki kiasi cha shillingi 40,000/=, then waulize urudi tarehe ipi kuja kuchukua leseni yako mpya, very simple
 
Back
Top Bottom