Jamani mi natarajia kumaliza chuo kikuu mwaka huu B.A in Marketing lakini ndoto yangu ni kujiajiri na si kuajiriwa ila sasa tatizo sielewi nianzie wapi kama mnavoijua elimu yetu. Nipeni somo wadau. Nipo Mwanza.
Mambo makuu ya kuzingatia:
1. Elimu Sahihi ya jambo unalotaka kulifanya, haijalishi lina udogo gani
2. Mtaji, si lazima uwe mkuuuubwa kihivyo lakini wa kuweza kutosheleza kuanza kwa biashara, mtaji ni kama mtoto, unakua au unaweza kupata utapiamlo.
3. Wazio la biashara ambalo unaona linaweza kukutoa kimaisha, hilo wazo ulipende na uwe tayari kuliboresha kila siku. Liwe limeandikwa kwa mfumo wa SWOT( Nafikiri unaelewa ni nini hiki)
4. Tambua mazingira utakayofanyia biashara yako.
5. Jiamini unaweza kufanya vitu vikubwa
kila la heri mkuu, for more info ni pm,ushauri bureeeeeeee,,,,