Msaada namna ya kujua faida kwenye duka

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
Kama nilivyosema Wanajf msinichoke.Bado naendelea na kaduka kangu nyuma ya genge kwani nilifanikiwa kufungua vyote viwili.Tatizo sijajua namna ya kupiga hesabu na kujua nimepata faida kiasi gani ILA NASHANGAA VITU VIMEONGEZEKA KWENYE KADUKA SI KAMA NILIVYOANZA!!!Kwani kila pesa ninayouza nanunua vitu.Nasubiri nyie wataalamu wa kukokotoa faida mnisaidie!!!
 
angalia bei ya vitu vyote unavyonuna then angalia bei unayouza ile tofaut sasa toa hela ya tra then inayobak toa kodi ya frame then toa mshahara wako unaojilipa then toa bili ya umeme toa na bili ya maji inayobak ndio faidaa...
 
Naendelea kusubr wataalam nipate ma ujuz na mm na vibiashara vyangu
 
Haya maduka ya mtaani ya kuuza unga na bidhaa zake ndogo ndogo si rahisi kujua faida,sema kadiri ya vitu vinavyoongezeka au kupungua ndio unaweza kusema unapata faida au hasara.
 
hapo labda cha msingi chukua daftar uandike kila kitu ulichonunua ulinunua sh.ngapi! then kila utakapouza andika...mwisho wa siku utajua kila kitu kimetoa faida ya sh.ngap, hapohapo utatoa kodi tra, kodi ya mlango, bill ya umeme ya maji, lesen ya biashara, fire xtingwisha, kodi za takataka, kadi ya afya, kuna na zile fain za uchafuzi wa mazingira[emoji6][emoji23]! ukishatoa vyote hivyo utajua faida yako...
 
WASILIANA NA MTU MMOJA YUKO HUMU ANAITWA "CONSULT" anaweza kukusaidia
 
Chukua gharama zote za uendeshaji kwa mwezi kisha gawa kwa siku 30. Gharama hizo ni kama vile usafiri wa mizigo, nauli yako ya kwenda kazini, maji, umeme, kodi ya duka, kodi za TRA kwa mwezi, kodi nyingine zote, nk. Kisha chukua mauzo ya siku moja toa hapo hiyo gharama ya siku na bei ya kununulia hivyo vitu ulivyouza siku hiyo. Itakayobaki ndiyo faida yako
 
Kwa mfano umenunua sabuni box1 40,000 gawanya kwa idadi ya miche iliyo kuwa ndani utajua kila mche unafaida sh ngapi then unakata vipande vipande ili kujua kila kipande una faida kiasi gani

Mf 40,000/25= 1600ndo bei ya mche mmoja uliouziwa so hapo uta jumlisha mf 400 ndo faida yako kwa io kwa kila mche mmoja ukiuza faida yako ni 400 unazidisha mara 25 idadi ya mche kujua faida ya box 400*25=10,000 kwa io katika box moja la sabuni faida yako ni 10,000
 
Hii ni ngumu sana ku'count uijue faida. Kwa sababu duka lina vitu vingi sana vidogo vidogo. Utahesabu vingapi? Vizuri kama mwaka wa kwanza usichukue chochote toka dukani. Mpaka tuka li'machue. After then utajua trend ya vitu kutoka dukani na movement ya kila bidhaa... Pia litakua limeji'multiply.... Then unachukua 10 to 15% kila cku kama faida.
 
Ok sawa mkuu vp umejuaje 10% ndo faida tupe nasi mchanganuo
 
Duu,kwa kukokotoa hivyo kaka bado ni mtihani.
 
Duu,kwa kukokotoa hivyo kaka bado ni mtihani.
biashara saiv ni ngumu jamani kwa huku kwetu cjui mikoa mengine! me pia nataka mlango wa duka km huyu mtoa mada! nafkiria sana chakufanya na haka kahela kangu lkn naona km sielewiiiiiii! nataka biashara angalau kwa siku nipate faida ya elfu kumi! itakuwa c haba kwangu! nachangaanyikiwa![emoji32]

Sent from my SM-G531F using JamiiForums mobile app
 
nakumbuka wakati mdogo tulikuwa na duka la vyakula, mama angu alikuwa anasema faida yake ni almost 20% kwa kila bidhaa ukiuza bei ya kawaida na kila kitu kikiwaa constant. Kwa hiyo ukiuza laki moja faida ni 20,000/. Sasa kwenye hyo asilimia 20 weka na pango...
 
Unachoweza kutambua ni mauzo yako..ni kiasi gani kwa siku...unachotakiwa kufanya chukua siku moja andik kila unachouza...angalia na gawanya gharama za uendeshaki kwa kila item...tofauti utakayopata.ukito manunuzi..hio ndio faida kwa kurahisisha..unaitafutia %kwa hio siku ukiuza kidogo 10000unazidisha na percentage yako unapata jibu hivyo hivyo ukiuza sana..kuna item zinazotoka taratibu hizo hauziinclude sana...
 
Ok sawa mkuu vp umejuaje 10% ndo faida tupe nasi mchanganuo

Rahisi sana, chukua bidhaa kadhaa kama sample, kisha piga hesabu ujue faida unayoipata kwa siku kwenye bidhaa hizo, then utajua hizo asilimia
 
Ni rahis saana. Sema watu wengi wanabwabwaja hawajui mwisho wa siku mtu kama una duka lina item zaiidi ya 70 tofauti utaishia kuhahaa tu[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji3][emoji3]
Fanya hiv
Hasa kwa duka huwa tunapiga hasa profit in anual( mwaka) basis..

Sales( mauzo yote ya kila siku ya mwaka) - Purchase ( manunuzi yote ya mwaka) = Gross profit
Ili kupata Net profit ambayo ujue mradi wako wa duka umekuingzia mpunga kiac gan then tafuta net profit

Net profit= Gross profit - All cost of running business nayo in anual basis + losses( hasara)..

FANYA STOCK TAKING ambapo utahesabu bidhaa zote ulizonazo dukan na thamani zake ili upate capital ulinayo kwa muda huo( KIlio sana kwa watu wenye duka la item nyingi[emoji2][emoji2][emoji2]) ili uweze kujua mtaji wako ni kiac gan na kama pia mtaji wako unakua au unashuka..

Naposema cost za businees zinacomprise:
●kodi za tra, fremu kama umepanga,maji, umeme, mishahara wanaokusaidia, n.k.. hata kma unaking'amuzi dukani kwako nayo ni cost ya biashara kama duka linakilipia
● hasara nazo zinakua calculated mf. Bidhaa zimeharibika, zimevunjika, zimeexpire, n.k hizo ni hasara lazima ziwe calculated.



Nb: usije ukachukua hela kwenye droo ya pesa ya kuuzia afu mwisho wa siku ukasahau kuongeza iyo pesa kama mauzo ya siku coz utaharibu mahesabu ya mauzo kila siku
Pili, hakikisha una daftari ( zuri zaid coz computer huwa zinacolapse sometimes) la kutunza kumbukumbu za baishara zote..ikiwemo gharama za baishaara, maingizo ya mali, mauzo n.k


Hapo nimetoa njia ya kawaida saaana ambayo siyo ngumu kiivo.. naimani utanielewa

Hiyo ya kusema ni asilimia ngap ya mauzo itabidi upate average ya percentage profit ya kila item then ukipata lets say 10% then utachukua 10% ya mauzo yako let say 200k kwa siku then gross profit itakua 20k.. kwa siku iyo.. kama una mauzo ya mwaka basi total ya mauzo ya mwaka mara 10% ndo itakua *gross profit* ie. Haina cost za biashara... hiyo ni roughly...sio accurate sana ila almost accurate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…