Msaada namna ya kujua faida kwenye duka

Maelezo mazuri sana ila ni lazima iwe kwa mwaka ? je akitaka kujua faida au hasara kwa kipindi kifupi kama wiki 3 na ana duka la reja reja lenye Items zaidi ya 120 ?
 
Maelezo mazuri sana ila ni lazima iwe kwa mwaka ? je akitaka kujua faida au hasara kwa kipindi kifupi kama wiki 3 na ana duka la reja reja lenye Items zaidi ya 120 ?
Tumia ya chini iyo ya average percentage profit ni shortcut moja balaa utapata hata faida ya siku 1 au week tuu mkuuu
 
Binafsi huwa Nna utaratibu wa Kurekodi mauzo.

Pia, nmeweka utaratibu wa kurekodi Matumizi

Huwa najitahidi sana Matumizi yangu yote ya siku yasizidi 10% ya Mauzo yote ya siku.

MF: Siku Nikiuza 1mil, huwa najitahidi sana Matumizi yangu yote ya Siku yasizidi laki 1.

Nb:
Matumizi yang yote ya Siku
Namaanisha ela ya kula, usafiri, umeme(nyumban&dukan),maji (nyumban&dukan), ada za watoto, gharama binafsi zangu,wazazi wangu,make wangu, watoto wangu Na ukweni, TRA, LESENI.

Kuhusu faida,
Aisee sijui, ila faida na hasara naiangalia kwa Uwezo wangu wa Kuagiza mzigo.

Yaan, Jinsi nnavoagiza mzigo mkubwa zaid ya ule uliopita ndo huwa najiona napata faida.

Nikijiona kasi ya kuagiza imepungua, aisee najiona napata hasara.

Nawasilisha
 
Biahara ndogo ndogo kma iyo ni vigumu kujua exactly faida au hasara unless unachooza unaandika.

Ila kwa urahisi tafta average profit unayopata katka vitu unavyouza. So kma ni 20%, yale mauzo yako ya kila siku unaasume 20% ndyo faida.( profit)...ila ukitaka kupata net profit ndyo unatoa zile fixed costs kma Tax, Rent na labor costs
 
Mkuu hiyo njia ni hatari kama huna control ya matumizi.. actually ile 10% ya mauzo naomba tuelewane apa sio applicable kwa kila bidhaa ni lazima upate average percentage profit ndo utaweza calculate Faida inayoonekana( gross profit) sio faida halisi ( net profit)
Mfano..
Nina duka lina item 3 tofauti

Cement nanunua 13k nauza 13,500 profit 4%
Rangi 20lt nanunua 28k nauza 30k profit 7%
Gypsum powder 15k nauza 16k profit 7%

Then kwa duka kama hili Average % proft = 4% + 7% + 7% divide by 3 unapata 6%

Kwaio mtu mwenye duka hili akiuza 150, 000 kwa siku then gross profit yake ni 150k × 6% = 9,000 ndo gross profit.

Jaman ni muhimu sana mahesabu ya mradi wako ili usitumie hela kuliko vile duka linaweza kutwngeneza.
 
Biashara nnayofanya Mimi, average profit ni 30%-50% kwa bidhaa zote

Hiyo biashara kama yako nliwahi kuifanya, mwanzoni nkaona hailipi nkaachana nayo.
 
Biashara nnayofanya Mimi, average profit ni 30%-50% kwa bidhaa zote

Hiyo biashara kama yako nliwahi kuifanya, mwanzoni nkaona hailipi nkaachana nayo.
Basi inamaa average % profit ni 40% ya mauzo yako wether ya mwez au siku..
Kwaiyo kama kwa siku unauza sh 500,000
Faida yako inayoonekana( gross profit) ni= 500,000 × 40% sh 200,000 kwa iyo siku
Apo ujue kwenye iyo lak 2 apo hujatoa daily cost za business ambazo kuna variable na fixed cost za business ambazo utaweza kuzikalculate siku iyo na kujua umezalisha faida halisi ( Net profit) kiac gan mkuu..

Nawasilisha
 
Hello....wakuu wangu poleni na majukumu ya kila siku .... IRINGA DECOR bado tunaendelea na ofa ya furniture mbalimbali katika msimu huu wa Xmas na mwaka mpya ....tutaendelea kutuma bei zetu rafiki kwa mtanzania wa kawaida .... Zifuatazo ni bei za makabati ya jikoni( kitchen cabinets) ,zikifuatiwa na bei za milango [emoji95]BEI ZA KITCHEN CABINET KWA MSIMU HUU WA XMAS NA MWAKA MPYA -Mbao aina ya mninga au mkongo [emoji91]940,000/=
BEI HII INAHUSISHA VITU VIFUATAVYO SIZE .Mita moja ya Kabati la chini na Kabati LA juu yote kwa pamoja , pamoja na marble **940,000/= kwa kila mita moja [emoji95]MDF PINE 525,000/= BEI HIYO INAhusisha mita moja Kabati LA chini na juu pamoja na marble [emoji91][emoji91][emoji91]MILANGO NA FREM ZAKE *MBAO ,MNINGA AU MKONGO 350,000/= *MBAO ..ZINGNEZO 265,000/= *JOINED BORD 325,000/= KWA HUDUMA ZA KITCHEN CABINETS TUNAKUFUATA MTEJA MPAKA ULIPO....milango tunafikisha mpaka ulipo kwa gharama zetu
KARIBUNI SANA KWA BIDHAA ZETU ZENYE UBORA WA HALI YA JUU Call/text/WhatsApp. 0657888724
 
Ni simple sana kujua kama unapata hasara au faida katika maduka ya rejareja ambayo ni ngumu kuhesabu bidhaa mojamoja.
Ukiamua utafanya kwa siku au kwa mwezi, ila ni vizuri ufanye kwa siku ili ujue trend yako.
Fanya hivi,
Jumla ya mauzo ya siku - (manunuzi ya siku + gharama ya usafiri) = faida ghafi au hasara ghafi. 500,000-230,000=270,000
Faida au hasara ya siku husika = faida ghafi - gharama za uendeshaji.
Gharama za uendeshaji ni kama kodi ya frem, kodi ya tra, mshahara, bili ya umeme wa dukani, na nyinginezo lakini hakikisha hizo gharama ni kwasababu ya biashara tu. Kama umetoa hela ya kula nyumbani hakikisha unajiandikia deni, ukichukua vocha ya kumpigia mchepuko jiandikie km deni.
Km baadhi ya gharama unalipa kwa mwezi, gawanya kwa 30 ili upate gharama ya siku ie kodi ya frem, mshahara nk.
Faida au hasara kwa siku ~270,000-170,000=100,000
Kama kuna siku umepata hasara usiogope, kesho au kesho kutwa itajirecover yenyewe shida itakuja km utafululiza kupata hasara siku nyingi mfululizo.
Faida za hii formula ni kuwa hauna haja ya kupiga mahesabu mengi sana kwasababu gharama nyingi zipo fixed incase kuna mpya umeiongeza.
Mwisho wa mwezi jumlisha faida au hasara ulizopata kila siku alafu utoe madeni ya kibiashara kwa mwezi huo.
So kwa mwezi utajua umeingiza faida au hasara kiasi gani
 
Kwanza natumai unaandika matumizi yako yote ya kila siku kuhusu hilo duka toka uanze.

Halafu kila unapofunga duka unahesabu mapato uliyoingiza siku hiyo na unayaandika.

Ukifunga baada ya kazi ya siku toa matumizi. Balance ndiyo faida au hasara mpaka siku hiyo.
 
Mkuu hii njia sio simple kama unavosema.. unless kama una duka dogo lenye bidhaa za aina chache au ni mradi duka ambao unabidhaa ambayo ni aina moja mf. Kuku au mayai..

Kwanini?
Nikiongelea kwa duka lenye item nyingi za aina tofauti mf. Ni hardware unauza nyundo, misumar, rangi za aina tofaut tofauti, cement , hard board, tuvifaa twa bomba ambavyo ndani yake tuna category, n.k . Yaan unakuta una item zaid ya 70 tofauti tofauti.

●Sasa itakulazimu kuandika kila unachouza ili baadae unavofanya mahesabu ujue umeuza bidhaa gan , zilinunuliwa kiasi gan kwenye daftari la manunuzi ili uje utoe na sales( mauzo ya siku) na cost za business.

kazi ambayo sio simple kuifanya daily ndo maana hua mahesabu kama haya na stock taking hufanywa kwa mwaka au nusu mwaka kujua maendeleo ya biashara yako.

● pia tuelewane pia hela uliyochukua wewe mwenye biashara ambayo umeitumia kwa matumizi yako binafsi haipo kwenye cost za biashara husika otherwise u have to count it as loss( hasara).
Wewe inatakiwa uangalie faida halisi( net profit) ndo utumie io hela ya matumizi binafsi chini ya hiko kiwango for further investment.


Nawasilisha
 
Mkuu hiyo nadhani upo sahihi kama unatoa biashara ya huduma na sio bidhaa..
Mfano biashara ya huduma ya choo ukifanya ivoo ua right mkuu
Ila kwa biashara ya bidhaa lazima ujue umenunua bidhaa kiac gan na mengine yafuate
 
Nafikiri ujanielewa vizuri ndugu,
Sijasema kila unachouza ukiandike, nimesema chukua jumla ya mauzo ya siku utoe jumla ya manunuzi ya siku hiyo (hapa unaweza ukapata negative kwasababu siku hiyo umenunua mzigo mkubwa sana lkn sitegemei upate negative kila siku coz haiwezekani uwe unanunua tu mzigo mkubwa kila siku) then utoe gharama za uendeshaji kwa siku husika.
Kuhusu kutoa hela dukani kwa matumizi yako binafsi au umemkopesha mtu, nimesema hiyo hela jiandikie wewe mwenyewe kama deni na endapo mpaka mwisho wa mwezi haujairudisha hiyo hela kwenye biashara basi jumlisha zile faida zako za mwezi mzima utoe hilo deni au hela uliyoichukua kwenye bss yako ndani ya mwezio, so hapo ndo utajua kwenye hiyo biashara kwa mwezi umepata sh ngapi au umepata hasara ya sh ngapi.(Actual net profit or Actual net loss.
Ukitoa hela kwenye biashara kwaajili ya matumizi binafsi (drawings) hauwezi ukahiita ni hasara, hasara ni umenunua kitu 5000 we ukaja kukiuza 4500. Sh 500 ndio tunaihita hasara.
 
Biashara nnayofanya Mimi, average profit ni 30%-50% kwa bidhaa zote

Hiyo biashara kama yako nliwahi kuifanya, mwanzoni nkaona hailipi nkaachana nayo.
Mkuu biashara gani hiyo yenye faida kubwa hivyo yaani 30-50% nipe mtonyo mzee baba!
 
Hayo mambo yenu ya vingereza vya Variable cost na Fixed cost

Ndo huwa yanawafanya wasomi mnashindwa kufanikiwa kwenye biashara, UOGA KIBAO.

Kumbe kiuhalisia,
hayana uhusiano wa moja kwa moja na maisha halisi ya biashara.
 
Hayo mambo yenu ya vingereza vya Variable cost na Fixed cost

Ndo huwa yanawafanya wasomi mnashindwa kufanikiwa kwenye biashara, UOGA KIBAO.

Kumbe kiuhalisia,
hayana uhusiano wa moja kwa moja na maisha halisi ya biashara.
Ha ha ha upo sahihi mkuu, msomi akitaka kuanza biashara au mradi wowote atakuambia lzm afanye research oh sijui acalculate risk za hiyo business oh sijui aandike business plan. Kitu kinachomkatisha tamaa mwenyewe. Wakati mtu wa kawaida akiona fursa ipo sehemu anairukia faster litakalokuwa na liwe atapambana nalo mbele ya safari
 
Mkuu biashara gani hiyo yenye faida kubwa hivyo yaani 30-50% nipe mtonyo mzee baba!

Uza mitumba Mzee, hapo wawezA pata hata 500% profits
Mfano Mtu kanunua nguo Classic kwa 15,000 akauza kwa 70,000/= hapo faida ni kama 366%
So kuna biashara nyingi tuu za more profits than ever
 
Naomba nikufate PM. Unisaidie. Thanks in advance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…