Ni simple sana kujua kama unapata hasara au faida katika maduka ya rejareja ambayo ni ngumu kuhesabu bidhaa mojamoja.
Ukiamua utafanya kwa siku au kwa mwezi, ila ni vizuri ufanye kwa siku ili ujue trend yako.
Fanya hivi,
Jumla ya mauzo ya siku - (manunuzi ya siku + gharama ya usafiri) = faida ghafi au hasara ghafi. 500,000-230,000=270,000
Faida au hasara ya siku husika = faida ghafi - gharama za uendeshaji.
Gharama za uendeshaji ni kama kodi ya frem, kodi ya tra, mshahara, bili ya umeme wa dukani, na nyinginezo lakini hakikisha hizo gharama ni kwasababu ya biashara tu. Kama umetoa hela ya kula nyumbani hakikisha unajiandikia deni, ukichukua vocha ya kumpigia mchepuko jiandikie km deni.
Km baadhi ya gharama unalipa kwa mwezi, gawanya kwa 30 ili upate gharama ya siku ie kodi ya frem, mshahara nk.
Faida au hasara kwa siku ~270,000-170,000=100,000
Kama kuna siku umepata hasara usiogope, kesho au kesho kutwa itajirecover yenyewe shida itakuja km utafululiza kupata hasara siku nyingi mfululizo.
Faida za hii formula ni kuwa hauna haja ya kupiga mahesabu mengi sana kwasababu gharama nyingi zipo fixed incase kuna mpya umeiongeza.
Mwisho wa mwezi jumlisha faida au hasara ulizopata kila siku alafu utoe madeni ya kibiashara kwa mwezi huo.
So kwa mwezi utajua umeingiza faida au hasara kiasi gani