Adilinanduguze2
JF-Expert Member
- Mar 11, 2014
- 1,386
- 1,919
Nadhani kitu cha muhimu hapa kama una kijana dukani lazima umpe taswira kwamba nature ya biashara mnayofanya haina kudharau pesa ndogo au kitu kidogo kama kibiriti au sigara lazima viwe recorded
Ukishamjengea nidhamu hiyo sasa ndio unakuja kwenye mfumo wenyewe wa kimahesabu
1. Matumizi yake ya kawaida kama Msosi ambayo tayari mnakuwa mmewekeana viwango
2. Matumizi ya kibiashara kama umeme, maji, bima, city levy, tra, license, nk
3.Withdrawals hizi ni pesa unazochukua wewe kwenye biashara ambazo kimsingi ni mkopo. Biashara yako inakudai
4. Mauzo, kama nilivyosema mwanzo lazima mauzo yarikodiwe kila mara yanapofanyika. Na kumrahisishia muuzaji unaweza kumpatia page ambayo ina list ya items zote ktk alphabetical order kupunguza kuandika andika kila anapofanya mauzo kwa mfano mtu anataka Sigara Sports 2 anamuuzia akimaliza anachukua karatasi yake kwenye Sigara Sports anaweka 2 hivyo hivyo kwa bidhaa zote
Mwisho jioni anajumlisha cash analinganisha na ile orodha yake anatoa na gharama alizolipia kwa siku hiyo then inabaki Balance ambayo ina tally.
Zoezi hili litafanyika kila siku jioni baada ya kufunga duka, kila wiki, kila mwezi, kila robo/nusu/mwaka mzima
Na kutakuwa na Daftari maalum la Mauzo na Matumizi
Ambapo itaandikwa 1. Aina ya bidhaa iliouzwa, 2. Idadi ya bidhaa zilizouzwa na 3. Bei ya mauzo. 4. Jumla ya Mauzo
5. Manunuzi, Shopowner anaweza jipangia kufanya manunuzi mara 1 kwa wiki au mara 2 au zaidi ya hapo Manunuzi yote lazima yafanywe ktk daftari maalum. Katika hilo daftari lazima iandikwe 1. Aina ya bidhaa zilizonunuliwa, 2 bei ya Manunuzi. 3 Jumla ya Manunuzi
6. Ulinganisho
Kila week, litachukuliwa Daftari la mauzo
1. Litalinganishwa na zile daily Sales sheets ambazo nilisema zitakuwa zinamsaidia muuzaji kurecord sales kwa haraka na kutoa matumizi ya siku hiyo ili kupata cash iliyokusanywa wiki nzima kama inalingana
7. Atachukua Daftari la Mauzo ataangalia idadi ya bidhaa zilizouzwa ataitoa katika idadi ya bidhaa zilizopo na kujumlisha bidhaa nyingine kama kuna manunuzi yamefanyika. Hapa kunaweza hitajika daftari jingine la stock. Katika hali kama hii ni rahisi kufuatilia stock randomly hata on weekly basis. Wiki hii mnaweza mkafanyia sampling let say Sigara, Vibiriti, Sukari, Majani ya Chai na Azam Cola.
Mnaweza chukua Daftari la Stock mkaangalia idadi ya hizo bidhaa mkachukua na Daftari la Manunuzi ili kuongeza idadi ya bidhaa kama kuna Manunuzi yoyote yamefanyika ktk hizo bidhaa 5. Mkachukua tena na Daftari la Mauzo ili kutoa au kupunguza idadi ya bidhaa zote zilizouzwa na kinachobaki ndio physically itabidi muangalie jee ni vibiriti vingapi vimebaki vinalinganaje na records zetu
Huwezi kuifanya hii process kila week kwa bidhaa zote lakini waweza ifanya kwa kwa bidhaa chache kama sampling ili kuwa na uhakika kwamba biashara iko under control sio hivyo tu itasaidia kumpa picha Muuzaji kwamba akifanya madudu ni rahisi kugundulika
Sent using Jamii Forums mobile app