Msaada namna ya kutatua changamoto hapo kwenye circuit breaker

Msaada namna ya kutatua changamoto hapo kwenye circuit breaker

Skythelimit

Member
Joined
Jul 19, 2023
Posts
61
Reaction score
133
IMG_20240805_225049_823_105526.jpg

Hello habari!
Naomba msaada hapo kwenye hiyo circuit breaker maana umeme umepata hitilafu kidogo ukajizima.
 
Fundi afuatilie mfumo mzima ajue lazima kuna shoti ya waya kugusana, au shoti ya circuit (kifaa cha umeme kina shoti, chomoa chomeka kifaa kimoja kimoja). Havells ni CB nzuri inatrip sababu kuna shida mahala. Pia angalia vifaa vyako wenda vina shida.
Kama CB itakuwa na shida achana na Havells chukua Tronic.
 
Kama hujui kabisa umeme bora uache kabisa, lala giza asubuhi tafuta fundi, umeme hauna adabu.

Au lah kwa haraka haraka, zima vifaa vyoote, kisha anza kuwasha kimoja kimoja, ikijizima kwa kifaa fulani basi huenda hapo changamoto ni hicho kifaa, au lah hizo njia washa moja moja, ikijizima basi kuna tatizo njia fulani, hiyo njia usiiwashe tumia hizo nyingine, kesho tafuta fundi arekebishe.
 
Mcb mbili apo zimejizima,pandisha hyo c10 na c18 maana ndyo zimebeba nyaya zinazowasha taa . Ukiona taa haziwaki achana napo tena ikibidi shusha kabisa na hyo circuit breaker leta fundi asubuhi
 
Kuna njia mbili hapo zinashida hazipati umeme, ita fundi atatue tatizo ndio uwashe au kama una juwa hilo tatizo limesababishwa na nini, ondoa hicho kifaa uwashe.
 
Shukran wote mliochangia uzi huu, niligundua ni charger ya mchina ndio iliniletea shida. Siitumii tena
 
Back
Top Bottom