thankx,jf ndo jibu halis,nimefarijka sana!,what iz the way foward?
the way forward ni kama ifuatavyo na kwa mpangilio huu hapa chini.
1- kaa na demu wako muambie upo tayari kuulea ujauzito na mtoto na yeye mama yake pia ili aachana na wazo la kuutoa ujauzito
2- anza kufurahia kitendo ulichokifanya na kujiona ni mwenye bahati na baraka za mungu zimekujia kupata mtoto wa ujanani na kuwa tayari kumlea rais mtarajiwa wa nchi yetu
3- kuonyesha ulivyofurahia kuanzia sasa jiite baba kijacho au baba-k ili tuwe kila mara tunakumbuka na wewe pia ukumbuke ujio wa mwanao huyo kijacho...na uwe unatupa update za maendeleo ya ujauzito maana ndio afya ya kijacho huyo tuliyemnusuru hapa jf.
4- acha kukaa vijiweni walikokutia kiburi cha kuanza kufikiria kuuwa mtoto kijacho...wanaweza kukuambukiza ujinga ukaja kumkimbia demu wako na kumtelekeza mwenzako naujauzito kisha akaamua kumtupa mtoto kijacho jalalani.
5- anza kuongeza kipato chako ikiwezekana kiwe mara dufu ya unachopata kwa sasa maana malezi ya mtoto nayo ni gharama.
6- tumbo la mama likifikisha miezi mitatu jilipuwe kwao na binti wakujuwe na usiende kisela na jinsi yako mlege kama umebeba kifusi cha kokoto mifukoni...vaa kistaarabu na uende na wazee watu wazima kama mie tukajitambulishe na kuomba radhi kwa kumwaribu mtoto wao ila sie wazee tutaahidi kuwa mara baada ya kujifungua lazma tuwapeleke church au sheikh achome ubani tumlaani sheiteani itawale amani.....
Angalizo...hapa katika hatua hii kwa mila za kiafrika lazma kunakupigwa faini au penalti...inabidi tuwe na kipa bora kama wa uholanzi....namaanisha mpunga utatumika.
7- kama ni mtoto wa skull.....na hasa hizi za msingi.....baba kuna wimbo mmoja aliimbaga babuu wa kitaa unaitwa kimbia fasta.....huo unahusika kama hatua ya awali maana utaishia kwa kina babu seya na nguza.
8- hatua nyingine ni za malezi ya ujauzito na zinatofautiana..kama mama kukuchukia tuu mama kukupenda kiasi hataki hata uende jobu nataka kukuona 24/7, mama kula udongo mama kula mkaa, amam kugoma kuoga miez hata miwili full kuwa mchafu na ukijipafyumu ndani hulali na mengineyo.
Ni hayo tuuuuu....