MSAADA:Namna ya kutofautisha yai la kienyeji na kisasa

MSAADA:Namna ya kutofautisha yai la kienyeji na kisasa

john johns

Senior Member
Joined
Feb 13, 2014
Posts
113
Reaction score
64
Wanajukwaa naomba mwenye kujua namna ya kutofautisha yai la kuku ni lipi la kisasa na ni lipi la kienyeji kwa kuliangalia tuuu mwonekano wa nje. Msaada tafadhali.
 
Mayai ya kienyeji huwa yana rangi hii
Z(3).jpg
2Q==(2).jpg

Mayai ya kizungu yapo hivi

images(21).jpg

Joseverest issa mweusi john johns
 
Yana kiini hicho cha njano ila yakichemshwa au kukaangwa hio njano inafifia wakati ya kienyeji njao inakolea zaidi

Mfano mzuri Angalia chips mayai za mitaan wengi wanatumia ya kisasa hivyo njano ya kiini inakua imefifia
Yeah ni kweli ila haya ya huku Tz ya kisasa naona hayana kiini cha njano
 
Yana kiini hicho cha njano ila yakichemshwa au kukaangwa hio njano inafifia wakati ya kienyeji njao inakolea zaidi

Mfano mzuri Angalia chips mayai za mitaan wengi wanatumia ya kisasa hivyo njano ya kiini inakua imefifia
True Numbisa
 
Unjano hauko sawa mkuu, tena kwa sababu moja kubwa, yai la kienyeji mara nyingi tunakula ambayo yame rutubiwa (yana kifaranga) na Unjano uliokolea ni ajili ya uwepo wa damu.., ilhali ya kizungu waga hayaja rutubiwa (hayana kifaranga) hivo yanakuwa hayana damu na mwisho wake yanapoteza ule Unjano uliokolea
 
Hapana si kweli,hapa ninapoishi kuna kuku wa kienyeji. Nishakula yai\mayai ya siku moja i mean yametoka kutagwa siku hio, u njano upo kama kawaida. Yai lenye kifaranga au dalili ya kifaranga huwa kiini ni chepesi sana hakishikan kabisaaa

Kingine mkuu yai la kizungu ndio linatoa kuku wa kizungu hivyo nalo lina rutuba pia na expire time

Kuku yeyote wa kisasa au kienyeji akila majani kwa wingi......kiini kinakuwa njano. Mayai ya kienyeji mara nyingi ni madogo na yana ganda jeupe.
 
Hua nachukia mayai ya kisasa sana ila nakua siwezi kutifautisha kabisa yani..nikikua natumia factor ya ukubwa na kuangalia rangi sema jana tuu nimeenda dukani nikaonyeshwa ya kisasa ndio haya na kienyeji ndio haya yani hata sikuona utofauti manake kwenye yale ya kisasa yalikuepo meupe na mengine sio meupe pia.
 
Hapana si kweli,hapa ninapoishi kuna kuku wa kienyeji. Nishakula yai\mayai ya siku moja i mean yametoka kutagwa siku hio, u njano upo kama kawaida. Yai lenye kifaranga au dalili ya kifaranga huwa kiini ni chepesi sana hakishikan kabisaaa

Kingine mkuu yai la kizungu ndio linatoa kuku wa kizungu hivyo nalo lina rutuba pia na expire time
Unabisha kimazoea mkuu, haya mayai tunayokula ya kizungu hayaja rutubishwa, uli ule yai la kizungu ambalo limerutubishwa itabidi uwe na kuku wa kizungu wanaoitwa 'breeders' hawa hupandwa na majogoo, hawa wapo tu kwenye company zinazojishugulisha na utotoleshaji wa hawa kuku wa kizungu wanaotuletea mayai ya kukaangia chips yani layers ambao wao hawapandwi ili kurutubisha mayai yao, so sisi tunakula yasiyokuwa na vifaranga

Mayai ya kienyeji ndo tuseme yanaweza kuwa na expires coz yana kifaranga ndani ila haya ya kizungu ambayo sio ya breeders yanaweza kukaa muda mrefu sana bila kuharibika kwa sababu hatana mtoto ndani.

Kitendo cha kusema umekula yai la kuku wa kienyeji siku lilipotagwa na kuwa na kiini cha njano, inadhiirisha kuwa hujui unachoongelea mkuu, kuku anaetaga kila siku lazima atoke nje akapandwe na jogoo ili arutubishe yai, so usidhani kuwa eti pale anapolalia ndio anarutubisha hapana, inaonesha una nia na kujua haya mambo na kubisha waga ni sehemu ya kujifunza, ila nikushauli ukipata muda pitia pitia Google utapata elimu nzuri juu ya hawa kuku wetu na mayai yao
 
Yai la kienyeji ni dogo lina Ganda jeupe/cream
Yai la kisasa ni Kubwa lina Ganda la kaki kaki
 
Kumbe mmepitwa na wakati kiini cha njano huletwa na kuku kula majani siku hizi kuku wakisasa wanapewa majani kwa wingi na unauziwa mayai bei ya kienyeji

Sent from my SM-G610F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom