Msaada: Namna ya Kutumia Submeter ya Umeme

Msaada: Namna ya Kutumia Submeter ya Umeme

Restless Hustler

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2017
Posts
5,150
Reaction score
20,025
20241226_082106.jpg

Hapo pichani ni Submeter ya Umeme niliyoikuta kwenye nyumba ya kupanga
Ina namba ya mita yenye tarakimu sawa na ya TaNeSCo.

Naomba kufahamu Inafanyaje kazi
 
Navojua ufaa sana kwa wapangaji,lengo lake kuu huwa nikuondoa utata katika matumizi ya umeme kati ya mpangaji na mpangaji mwenzake,ili yoyote asionewe,alipe hela kulingana na matumizi yake.
 
Hiyo kitu inawekwa mnapokuwa na mpangaji zaidi ya mmoja, heshimu majirani zako, technology isikudanganye. Uliza wenyeji zako.
 
Navojua ufaa sana kwa wapangaji,lengo lake kuu huwa nikuondoa utata katika matumizi ya umeme kati ya mpangaji na mpangaji mwenzake,ili yoyote asionewe,alipe hela kulingana na matumizi yake.
Ninaponunua umeme natunia namba za mita hii ndogo au Ile ya TaNeSCo?
 
Hiyo sub meter inatumika kusoma matumizi ya umeme kwenye chumba chako, ukinunua umeme wa elf kumi, yenyewe itasoma unavyotumia, ni nzuri sana kwa wapangaji unalipa ulichotumia.

Namna ya kusoma.
ukinunua umeme record Unit ulizopata, mfano ni unit 28, hiyo meter itaanza kusoma namna unavyotumia mpaka zinapofika unit 28 unajua umeme uliobuniwa umeisha. binafsi nilinunua umeme wa elf10 mwezi wa tatu, nimekuja kununua umeme wa elf 10 tena mwez wa tisa
 
Hiyo sub meter inatumika kusoma matumizi ya umeme kwenye chumba chako, ukinunua umeme wa elf kumi, yenyewe itasoma unavyotumia, ni nzuri sana kwa wapangaji unalipa ulichotumia.

Namna ya kusoma.
ukinunua umeme record Unit ulizopata, mfano ni unit 28, hiyo meter itaanza kusoma namna unavyotumia mpaka zinapofika unit 28 unajua umeme uliobuniwa umeisha. binafsi nilinunua umeme wa elf10 mwezi wa tatu, nimekuja kununua umeme wa elf 10 tena mwez wa tisa
Ahsante Sasa mkuu
 
TUJIFUNZE ZAIDI JUU YA SUB-METER ZINAZO KATA UMEME.
Soma kwa makini utaelewa kitu’
Ninapo zungumzia SUB-METER nina maanisha kifaa kinacho pima na kukupa idadi ya kitu au matumizi ya aina tofauti sasa hii ninayo zungumzia hap ani SUB-METER ya umeme
Ila kitu muhimu ni kujua kuna aina mbili za sub-meter ambazo ni
SUB -METER YA KUHESABU UNIT na
SUB-METER ZA KUTUMIA UNIT ULIZO NAZO KAMA (LUKU)
#Kuna ORIGINAL na kawaida KULINGANA NA maitaji ya mteja
Nikianza na sub meter za kuhesabu unit
Hizi ni mita za umeme maalum kwaajili ya kuhesabu unit tu. Inamaana kama katika nyumba kuna wapangaji wa tatu(3) wana tumia (LUKU)moja kila mtu atahesabiwa unit kutokana na matumizi ya yake binafsi (personal user) ambayo ukiwa na hizi auna limiti ya kumkatia mwenzako umeme badala yake atakama atoi pesa ya umeme ataendelea kutumia umeme wa wapangaji wengine pasipo kua na kizuizi chochote.
Lakini sub meter hizi za KUSOMA unit zimekua na changamoto kwa watu kwasababu wengi wanalalamika awazielew na pia zinachanganya ki mahesabu na inakulazimisha kutunza kumbu kumbu za unit unazotumia na kingne azisaidii sana kwa wale wapangaji wanao kua watata katika kulipia bili ya umeme
Sub-meter za KUTUMIA UNIT ULIZO NAZO KAMA (LUKU).
Hizi ni sub meter maalum ambazo zimefungwa rilei (Relay- hiki ni kifaa cha umeme kinacho fanya kazi kama switch) amabayo inakuwezesha kutumia kama luku ya tanesco ya kawaida ila hii inafanya kazi pamoja na luku ya tanesco
UFANYAJI KAZI WAKE
Aina tofauti na luku ya tanesco kama nilivosema ila hii inafanya kazi na luku ya tanesco kama meter kuu
Kwa mfano
Nina wapangaji wa 4 kwenye nyumba moja na tunatumia LUKU MOJA YA TANESCO
Kinacho fanyika kama kwa kila chumba nikafunga sub meter ya kutumia unit. Kama kwenye LUKU KUNA UNIT 40 mnao uwezo wa kugawana uni 10 kila mmoja
Na ikitokea katika mgawanyo huo wa unit kuna mmoja ametumia zake zimeisha bc umeme unakata kwake tu pasipo kuwa buguz watumiaji wengine na ikitokea anaitaji umeme italazimika aweke kwenye luku kubwa ili aweze kupata halali ya unit zake alizo weka tena (ata kawiwa kwa kiasi alichoongeza)
UGAWAJI WA UNIT
KATIKA HIZI sub meter TUNAPOKUFUNGIA LAZIMA UPEWE ACCOUNT AMBAYO IKO KATIKA MFUMO WA WEBSITE yaa ni utapewa USER NAME NA PASSWORD ambayo hyo account itakuwezesha kugawa unit katika hizi sub meter zingine ambazo ziko katika link (zilizo unganishwa na hyo luku) inamaana utakapo weka umeme kwenye luku ya tanesco ili ugawiwe unit zako ni lazima mtu alie kabiziwa hii account aingie na achague kiasi cha unit ulizo weka katika luku ya tanesco akisha chagua ile account itakupa token ambazo utaingiza katika sub meter yako na utakua unatumia umeme ulio lipia.
KWA MASWALI NA MSAADA inbox me.
 
Back
Top Bottom