Kama utapenda pia waweza jifunza jinsi ya kutengeneza cottage cheese nyumbani bila kutumia mashine yeyote.
1. Andaa maziwa fresh lita 1
2. Andaa mtindi nusu lita
3. Changanya hayo maziwa fresh na mtindi ktk chombo kimoja, koroga na uyafunike.
4. Acha huo mchanganyo wa maziwa fresh na mtindi kwa saa 24
5. Baada ya saa 24 Chukua huo mchanganyiko wako na uuweke jikoni kwa saa 1
NB. Hakikisha maziwa yanapata moto na yasichemke. Hii ndo sehemu ngumu ya kuhakikisha maziwa yapo na moto wa kutosha lakini hakikisha hayachemki.
6.Baada ya saa 1 utaona cottage cheese ikielea ktk maji ya njano.
7. Wacha ipoe
8. Chuja hayo maji ya njano kwa kutumia chujio...mfano chujio la chai.
9. Sasa cottage cheese yako iko tiyari kwa matumizi
Unaweza kula cottage cheese kwa vitu vingi...mfano chapati za maji nyembamba zilizochomwa bila mafuta ama kwa mafuta kidogo ikawekwa na cottage cheeze pamoja na asali hufanya asubuhi yangu iliyochangamka.