Msaada: Naomba kufahamishwa mapungufu ya Mitsubishi Outlander

Scolari

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2017
Posts
1,721
Reaction score
2,383
Niko katika research yangu ya gari nzuri kwa sababu si muda mwingi nitamiliki.

Nimeitazama hii Mitsubishi Outlander imenivutia kimuonekano na uwezo wake wa kubeba raia kwa maana ya wingi wa seat.

Yapi mapungufu yake na changamoto zake?

 
Sina uzoefu nazo ila nimewahi kusikia kuwa kwa haoa kwetu upatikanaji wa spare zake ni changamoto sambamba na bei ya spare! Kama una connection nzuri ya kuzipata sio ishu sana maana ni gari kubwa with very low price! Hasa hiyo model uliyoweka nadhani ni ya 2008 hiyo
 
Achukue gari, dunia kama kijiji
 
Sawasawa Boss
 
Route za mjini
Mara chache mwanza-Dar mwanza-Manyara, Arusha na Moshi
Kwa uzoefu wangu mdogo wa magari Mitsubishi wanafail sana kwenye gari ndogo kuanzia kipindi kile cha Mitsubishi RVR. Gari SUV imara kwa Mitsubishi ni Pajero hasa zile za zamani. Hizi za kisasa sina imani nazo sana
 
Sio kweli mkuu, Mitsubishi ni gari nzuri sana na Imara kuliko hata Toyota. Ninamiliki Mitsubishi L200 Spotero D.I.D na L200 kavu mwaka wa 8 huu. Pia Nina Toyota Hilux D4D so Nina uzoefu na nilichoandika
Kamanda moshi embu share zaid. Hizo outlander na rvr kwa barabara zetu za kiafrika zina perform vizuri kweli?
 
Outlander ni gari nzuri sana hapa napoandika nimetoka kuichukua, aseee nukichelewa sanaaa.

Music bomba, HP kubwa.
Hongera mzee,

Ila kila kitu huwa kinakuwaga machachari wakati wa kuanza, ila kikisha kaa, ndio unaanza kuona machungu yake

Labda, pengine ungesubiri hata 3 months hivi atleast ndio uturudie na mrejesho
 
Hongera mzee,

Ila kila kitu huwa kinakuwaga machachari wakati wa kuanza, ila kikisha kaa, ndio unaanza kuona machungu yake

Labda, pengine ungesubiri hata 3 months hivi atleast ndio uturudie na mrejesho
Nimekuelewa mkuu, ila sijaagiza kwa kukuruupuka kuna rafiki yangu anayo muda sana na iko poa miaka minne sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…