Mkuu RS ni package tu katika brands za magari kama ilivyo LT, LX, LS au XLE. Sijajua uliona katika gari gani na ni katika body au katika front grill. Kama katika body ni package ya ndani ya gari ila kama katika grill, wengi wanaweka kama pambo tu.
RS kirefu chake ni Rally Sports au "Rennsport" in German. Utaona sana katika magari kama Audi, Posche na sports cars nyingine.
Toyota nae ana version za RS kama Vitz RS ambayo ni Vitz ya kawaida iliyokua modified na Toyota Racing Development (TRD).