palesh pizoo
Senior Member
- Apr 14, 2018
- 131
- 223
Wakuu nawasilimu.
Samahani na poleni kwa majukumu, naomba niende kwenye point. Kuna mzee wangu alikuwa na mwanamke aliyeishi naye kinyumba(Kama wapenzi) tangu 2009 bila ya kufunga ndoa (alitoa pesa ya barua tu) na wakadumu kwa muda wa miaka mitano wakiwa pamoja had mwaka 2014 yule mwanamke aliamua kuondoka mwenyew pale nyumbani kwa yule mzee akiwa hajaunda kitu chochote cha kudumu na yule mzee.
Maisha yaliendelea na yule mzee akapata ustaafu mwaka 2016 baada ya kustaafu akaoa kisheria kabisa mwanamke mwingine ambye anaishi naye hadi sasa. Shida imetokea mwanzoni mwa mwaka huu yule mwanamke aliyeondoka 2014 ambaye hakumwoa kisheria amefungua kesi kuwa anahitaji huduma au fidia kwa muda aliokuwa anatumika kwake alipwe fidia. Ombi langu kwenu wakuu naomba kujua kifungu kipi kinamruhusu huyu mama kuomba fidia hali ya kuwa hakumwoa kisheria na huyu mzee hakumfukuza na hawakuunda mali yoyote ile na hawajazaa hata mototo mmoja?
MSAADA WENU TAFADHALI.