Hapo, ni kuwasiliana na watu ambao, kama wewe unavyojaribu kuimba, nao pia wanajaribu au walijaribu kutengeneza muziki. Sio rahisi kukutana na mtaalam kabisa maana hatakua tayari sana kukupa muda wake na resources zake bure. Wapo watu wanaochezacheza au waliochezea DAWs kama cubase, abelton, reapear, logic, fl studio, cakewalk nk. Hao unaweza
1. kuwatumia audio, (uliyojirekodi kwenye simu)
2. ikajaribiwa beat,
3. ukapelekewa beat ukasikiliza kwa headphone huku unarekodi tena audio hiyohiyo ikiwa inayoendana beat (kwenye simu)
4. ukatuma audio inayoendana na beat, na iliyo kwenye ufunguo, ikaunganishwa.
Inaweza isiwe na ubora sana lakini ni hatua ya "kujaribu" na haina usumbufu. Maana kila safari huanza na hatua ya kwanza.
Unaweza kunicheki pia kama niliyewahi kujaribu. Ila usiwe na haraka sana, maana mambo hayo yanahitaji muda, na muda nao ni tatizo maishani