Msaada: Naomba wazo la biashara ambalo halitaathiri masomo yangu

Great_whiz

Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
19
Reaction score
29
Habari JF,

Mimi ni mwanachuo ninaesoma chuo fulani hapa Dar es Salaam, naomba ushauri wenu wapendwa. Yeyote mwenye wazo zuri la biashara ambalo haitoathiri muda mwingi wa masomo naomba nijue, na mtaji wake ni kiasi gani ili niongeze kipato changu na kupata uzoefu wa biashara kabla sijamaliza chuo, ili nisiwe tegemezi.

Ahsanteni sana, karibu kwa ushauri [emoji120][emoji120]
 
Chupi za kike chuoni mtaji hauzidi laki moja inatosha kabisa.. Faida ni zaidi ya mara mbili ya mtaji
 
Ahsantee sana kaka nitalifanyia kazi[emoji120]
 
Jikite katika namna ya kuweza kuwasaidia wanachuo kufanya assignment zao. Kama vile typing, editing maana wana chuo wengi wavivu na wanapenda bata.

Biashara za online mfano simu, nguo, chupi viatu, karanga na mengineyo wengi wanafanya unaweza fanya pia.

Jitangaze
 
Hili ndio wazo bora zaidi,kuna mdau wangu mmoja alikuwa anawafanyia assignments wamafunzi wenzake alikuwa anapiga hela.
Pia simu na laptops ni rahisi kuuza na ni rahisi kubeba unatembea nazo kwenye begi tu any time
 
Nicheki pm niwe nakuuzia laptops na simu from Dubai kwa bei rahisi unawauzia utawapata wengi tu.
 
Ahsantee sana mkuu Mungu akubariki hili ni bonge la idea aisee[emoji120]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…