Msaada: Napata changamoto ya ku-login NACTEVET akaunti

Wasomba

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2016
Posts
418
Reaction score
568
Naomba msaada, nimekamilisha kujiunga na kulipia NACTEVET kwa ajili ya application ya diploma. Tatizo linakuja Kila nikitaka kuloqin naambiwa nimekosea username au password ukizingatia username ni namba yangu ya mtihani. Mbaya zaidi nikijaribu option ya kuset password naye inakataa. Mbaya zaidi na zaidi nikiwapiqia simu awapokea.

Mbaya zaidi na zaidi yake nikiwaandikia email wananipatia namba ya simu ili niwapigie ambapo nikipiqa hawapokei. Mbaya kuliko zote nikiwaandikia email kuwajuza kuhusu simu yangu kutopokelewa wananiambia 'piga sasa'. Mbaya zaidi ya zaidi na kubwa kuliko zote ukipiga hiyo sasa hawapokei tena.

Naipenda nchi yangu Tanzania.

 
Kama upo dar nenda ofisini kwao. Hii nchi huwa wanakawaida ya kuweka mawasiliano lakini ni shida tupu. Taasisi nyingi za serikali wakitoa namba za simu ukipiga na ukafanikiwa kuwapata ni bahati sana. Yaani wangekuwa kama mitandao ya simu tungekuwa mbali sana. Pole kwa changamoto ila kama uko Dar nakushauri nenda ofisini kwao.
 
Huo ni uzembewako,na wazembe dawa yao ni system!
Acha kufanya vitu kwa pressure ndomana mnakoseakosea!
Umekosea mwenyewe unalalamika mwenyewe!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…