Msaada: Napata maumivu makali sehemu ya haja kubwa kiasi cha kushindwa kukaa

ZIna shida gani kwa kesi ya bawasiri mkuu?
Sababu kubwa ya constipation ni ulaji wa vyakula vyenye kiasì kidogo mno cha kambakamba/nyuzinyuzi (fibers), na mara nyingi kwa mijini culprit ni chips.

Kama mtu anakula mbogo za majani na matunda kwa wingi, nafaka nzima (zisizokobolewa), anakunywa maji ya kutosha, siyo rahisi kukumbwa na bawasili
 
Ulaji wako upoje?
 
Jaribu kuchunguza huwenda ni hemorrhoid grade 1
 
Kula papai, parachichi au juice ya Ukwaju
 
Inaweza kuwa hiyo bawasili ( haemorrhoids ) kama wengi walivyo sema hapo juu. Lakini pia inaweza kuwa shida nyengine inaitwa anal fissures. Hizi haemorrhoids na anal fissures hufanana kwa kiwango kikubwa sana dalili zake.

Fata ushauri ambao umeelezwa na wenzetu hapo juu. Lakini Mimi nashauri Kama utaweza ufanye kipimo cha colonoscopy. Kupitia kipimo hicho tutapata majibu ya uhakika zaidi kuwa ni anal fissures au haemorrhoids na itarahisisha zaidi matibabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…