Msaada: Napata maumivu makali sehemu ya haja kubwa kiasi cha kushindwa kukaa

Ishu ya kawaida sana japo wazee WA fursa wanawapiga Sana watu hela,Fanya hivi Kula mapapai Kwa wiki mfululizo na maji ya kutosha hakikisha unatoa mkojo mweupe kila siku Kwa wiki nzima! Papai Kula asubuh na jioni itapotea na hiyo ndio solution ya kudumu, ni ishu ya constipation ambayo chanzo chake ni kuto pata maji ya kutosha mwilini
 
Pole sana!
Maumivu kwenye njia ya haja kubwa husababishwa na vitu vingi. Moja ni hiyo kupata choo kigumu (constipation), kuwa na uvimbe sehemu ya haja kubwa mfano bawasiri (hemorrhoids), aina fulani ya minyoo, kuumia au kuumizwa sehemu ya haja kubwa, michubuko nk.

Ni vyema ukajikagua mwenyewe sehemu yako ya haja kubwa kuona kama kuna uvimbe wowote (bawasiri) au michubuko au ukienda kwa daktari akukague na kuangalia sehemu hizo sio kupima tu haja kubwa.

Kupata choo kigumu nayo kuna visababishi vingi, mfano ulaji wa vyakula vigumu bila kunywa maji mara kwa mara, (ulaji duni), kukosa mlo wenye mboga za majani na matunda (roughage, fiber rich diets), matumizi ya aina fulani za dawa/madawa, kukosa mazoezi, kupata maambukizi ya aina fulani ya bacteria 🦠 nk.

Kwa hiyo nakushauri ujikague sehemu yako ya haja kubwa na uende hospital kwa daktari akukague zaidi ili upatiwe matibabu ya tatizo litakalobainika.
Pole sana!
 
Pole sana mkuu hiyo Hali inatesa sana.Fuata ushaur uliopewa na watu humu na pia jitahid kunywa yoghurt na mboga zamajani kwa wingi.Hiyo hali inaweza kupotea na kurudi tena ukiendelea na ulaji mbaya
 
Kula mapapai kwa wingi
 
Kunyweni maji wajameni, kuleni matunda wajameni.

Bila maji lazima upate shida kupata hiyo starehe.
 
Bawasir hiyo kaka dawa ninayo nauza elf 50 ila kwa wadau wa jf ni elf 30 nakuletea mwenyewe mpaka kwako kaka 0712505049
 
Aisee pole sana.
 
Rudi tena hospitali tofauti, kubwa ikibidi. Inaelekea ukikoenda mwanzo wamepima kinyesi na hawakukuchunguza wewe
 
Ushapata dawa?
 
Mkuu pole sana. puka ushauri wa kutumia dawa bila kujua tatizo linasababishwa na nini. Rudi hospital na hakikisha unakwenda hospital yenye kueleweka na wana madakta wazuri.
 
Kwa maelezo ya mleta mada ni Kuwa ameenda Hospitali,na hiyo ni kusema kwamba ameonana na Daktari kama sio Madaktari,hivyo kabla ya kumshauri jiulize huko Hospitali alipopita hakushauriwa hayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…